News Update: Mgombea Ubunge Kinondoni CUF Awataka Wakazi Wa Kata Ya NDUGUMBI Msifanye Makosa Terehe 17
Mgombea Ubunge Jimbo La kinondoni CUF
Bw. RAJABU SALUM Akifafanua jambo kwa wakazi wa MAKANYA kata ya NDUGUMBI katika
mkutano wa kampeni za uchaguzi wa marudio jimbo la kinondoni.
Mgombea Ubunge Jimbo La kinondoni CUF
Bw. Rajabu Salum (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi CUF (katikati) Abdul Kambaya na katibu Mkuu wa Bodi ya
wadhamini Bw, Thomas
Malima na Katibu wa JUKE Taifa Bi, Salama Masoud wakiimba wimbo wa chama kabla ya kuanza mkutano katika kampeni
za uchaguzi mdogo wa marudi jimbo la kinondoni kata ya Ndugumbi Jijini Dar es
salaam.
Mgombea Ubunge Jimbo La kinondoni CUF
Bw. Rajabu Salum akibadilishana mawazo na Mkurugenzi
wa mipango na uchaguzi (NMCO) wa Chama cha Wananchi CUF Bw. Mneke Jafari (kushoto) katika kampeni za uchaguzi
mdogo wa marudi jimbo la kinondoni kata ya Ndugumbi Jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Wakazi wa kata ya wakazi wa makanya kata
ya Ndugumbi wametakiwa kutokufanya makosa tarehe 17 kwa kujitokeza kwa wingi siku
hiyo kwenda kupiga kura.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni katika
kata ya kata ya Ndugumbi mgombea ubunge
kupitia chama cha wananchi CUF Bw. Rajabu Salum alisema Kwa mujibu
wa takwimu alizonazo tayali chama icho kimeshajiakikishia ushindi katika jimbo
hilo kwa zaidi ya silimia 56 .
“Wakazi wa kata hiyo kujitokeza kwa
wingi siku hiyo kupiga kura kwani kwa mujibu wa takwimu tulizonazo mpaka hivi
sasa tayali tumejishajihakikishia ushindi kilichobakia ni nyie wakati
kujitokeza kwa wingi siku hiyo kupiga kura” Alisema Bw. Salum.
Bw. Salum amewataka wakazi wa kata hiyo
kutokuwa na wasiwasi juu ya kura zao kwani tayali wameshajipanga kuhakikisha
wanazuia hujuma zote zikazofanywa juu ya
chama hicho ikiwepo kuandaa wasimamizi makini ambao watasimama kidete kipindi chote
cha kupiga na kuhesabu kura.
Aidha Mgombea huyo aliongeza kuwa wananchi
wa kata hiyo kuwa makini na baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimekuwa
vikijitangaza katika majukwaa kuwa Chama hicho bado kina ushirikiano na vyanma
ivyo ( UKAWA) kuwa wawapuuze kwani CUF aina ushirikiano na chama chochote
katika uchaguzi huo.
Uchaguzi wa marudio wa jimbo la
kinondoni unatarijiwa kufanyia tarehe 17 mwezi kufatia alikuwa mbunge wa jimbo
hilo kujiuzuru ubunge na kujivua uanachama na kuamia CCM.
Baadhi ya Wakazi wa MAKANYA kata ya NDUGUMBI
wakifatilia hutuba ya mgombea Ubunge Jimbo La kinondoni CUF Bw. RAJABU SALUM
(hayupo Pichani)
No comments