Prof. Palamagamba: Aya Ndio Mamlaka Ya Rais MAGUFULI Kuhusu ZANZIBAR
Waziri wa katiba na sheria Profesa.
Palamagamba Kabudi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Magufuli ana mamlaka yote ya kutoa maagizo kwa Mawaziri ambao wapo ndani ya
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri Kabudi ametoa ufafanuzi huo
leo (Jumanne) katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea
mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Juma
kombo Hamadi alipotaka kufahamu Rais Magufuli ana mamlaka gani kikatiba ya
kutoa maagizo kwa Waziri aliyepo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
"Rais wa Muungano wa Tanzania
anayo mamlaka ya mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama
nchi huru", amesema Prof. Palamagamba.
Pamoja na hayo, Prof. Palamagamba
ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa "katika masuala yote yanayohusu
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkuu wa nchi ni mmoja tu tena ambaye ni Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli na yeye peke yake ndio Amri Jeshi. Hakuna mtu
mwingine yeyote wa kuyaamuru majeshi ya Tanzania isipokuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa sababu yeye ndio kiongozi mkuu wa serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania".
Kwa upande mwingine, Prof.
Palamagamba amesema Rais wa Zanzibar ni wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
mwenye heshima na hadhi ya urais kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano
yanayohusu Zanzibar ambapo pia ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa nafasi yake hiyo.
No comments