Jaji Mkuu Akamatwa Na Polisi.
Polisi nchini
Maldives imemkamata Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu nchini humo huku mgogoro wa
kisiasa ukiendelea kuwa katika hali mbaya kwenye nchi hiyo iliyoko katika
bahari ta Hindi.
Jaji Mkuu Abdulla
Saeed na Jaji Ali Hameed, walikamatwa na polisi baada ya nchi hiyo kutangaza
hali ya hatari huku kukiwa hakuna maelezo yaliyotolewa na uchunguzi au
mabadiliko juu ya mtafaruku huo ulipata kasi baada ya rais wa nchi hiyo Abdulla
Yameen alipokataa kutii amri ya Mahakama ya kuwaachilia wafungwa wote wa
kisiasa.
Maldives ni taifa
dogo katika bahari ya Hindi likiviunganisha visiwa vidogo 1,192 na utalii ndiyo
chanzo kikubwa cha mapato ya nchi hiyo. Wiki iliyopita Mahakama ya juu nchini
humo iliamuru kuachiwa kwa wanasiasa wa upinzani na pia Mahakama hiyo iliamua kwamba
mashitaka ya rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Nasheed ya mwaka 2005 ambaye
yuko uhamishoni yalikuwa kinyume na katiba.
Hatua hiyo ya
Mahakama ya juu ilifuatiwa na tamko la Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye
alisema kuwa atatekekeleza amri ya Mahakama na mara baada ya kauli hiyo
kamishna huyo alifukuzwa kazi na Rais Adulla Yameen huku jeshi la nchi hiyo
likiamuriwa kukataa kumuondoa Rais Yameen madarakani.
No comments