Mgombea Udiwani Wa CHADEMA… Ahamia Ccm Siku 3 Baada Ya Kuzindua Kampeni
Chadema
kimepata pigo baada ya mgombea wake wa udiwani Kata ya Manzase wilayani
Chamwino Mkoa wa Dodoma, Mashaka Chalo kujiunga na CCM pamoja na wanachama
wengine 131.
Chalo
amehama Chadema siku ya tatu tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini
kuzindua kampeni katika Kata hiyo na kunadiwa jukwaani na mbunge wa viti
maalum, Kunti Majala.
Uchaguzi
wa ubunge jimbo la Siha, Kinondoni na katika Kata 10 nchini utafanyika Februari
17, 2018. Uchaguzi katika Kata hiyo unafanyika baada ya aliyekuwa diwani, Peter
Madanya (CCM), kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.
Mgombea
huyo amehamia CCM jana Februari 4, 2018 katika kijiji cha Manzase wakati wa
uzinduzi wa kampeni za chama hicho na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Bara), Rodrick Mpogolo.
Mbunge wa
Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema uamuzi wa Chalo kujiuzulu ni ushindi
kwa chama tawala.
“Mpogolo
unaweza kufungua kampeni hizi na kisha kuzifunga maana kazi imekwisha. Tulikuwa
na wagombea watatu, lakini kuondoka kwa huyu, CCM tunaona kazi imekwisha.
Wagombea wengine waliobaki hata tukilala usingizi hakuna kitu ushindi ni wetu,”
amesema.
Mgombea
wa CCM katika Kata hiyo ni Amosi Mloha.
Lusinde
amesema Chadema walimpitisha Chalo dakika za mwisho kuwania udiwani bila kujua
kuwa alikuwa pandikizi la CCM.
Akizungumza
katika mkutano huo Chalo amesema amerejea CCM kwa sababu ni chama chake na
kimemlea.
Na Habel
Chidawali, Mwananchi
No comments