PICHA : Mazishi Ya KINGUNGE Yawakutanisha Viongozi Mbalimbali.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na
Marais wastaafu wa Tanzania na viongozi mbalimbali,wakiwa katika shughuli
maalum ya kumpumzisha aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale
Mwiru,makaburi ya kinondoni Dar es salaam.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiweka
udongo kwenye kaburi la muasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe Kingunge
Ngombale Mwiru ambaye anazikwa leo katika makaburi ya KInondoni Jijini Dar es
salaamMarais wastaafu,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete,Benjamin William Mkapa na Ali
Hassan Mwinyi wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mwanasiasa nguli na
mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru katika makaburi ya kinondoni Jijini Dar
es Salaam.
Viongozi wa Serikali walio madarakani
na wastaafu wakiongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wamejumuika na
waombolezaji wengine kuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu
Kingunge Ngombale Mwiru.
Shughuli ya kuaga mwili wa Kingunge
imefanyika leo Jumatatu Februari 5,2018 katika viwanja vya Karimjee, Dar es
Salaam.
Viongozi wengine walioaga mwili wa
Kingunge ni marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa aliyeambatana
na mkewe Anna; Makamu wa Rais mstaafu, Dk Mohamed Gharib Bilal; mawaziri wakuu
wastaafu Dk Salim Ahmed Salim, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na mkewe
Regina; na Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara), Philip Mangula na mtangulizi wake Pius Msekwa; Jaji Mkuu mstaafu
Mohamed Othman Chande; Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na
mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.
Pia, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Humphrey Polepole; Mama Maria Nyerere; Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye; na
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba.
No comments