Waziri Wa Kilimo Dkt Tizeba Amtumbua Mkurugenzi Mkuu Wa Bodi Ya Sukari Nchini.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt
Charles Tizeba
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu
wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara
moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia
leo Novemba 9, 2017.
Kwa agizo hilo
lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea
kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya
kupangiwa kazi nyingine.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza
Simwanza anasimamishwa
kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya
Sukari kutoridhisha.
Simwanza amehudumu katika
nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.
No comments