Meya Mwita Ahudhuria Mkutano Wa Mameya Duniani Nchini Ujerumani
Na Christina Mwagala, Ofisi Ya Meya Wa Jiji
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameondoka
Nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea Nchini Ujerumani kuhudhuria mkutano wa
mameya wote Duniani unaofanyika nchini humo.
Meya Mwita ameondoka Nchini hapa akiwa ameambatana na
Mkugenzi wa jiji Spora Liana ,Afisa Mipango miji wa jiji, ambapo watakuwa
nchini humo kwa muda wa siku nane na kurejea jijini hapa Novemba 15.
Meya Mwita amehudhuria mkutano huo wenye lengo la
kujadili suala la mabadiliko ya tabia ya nchi hususani katika kukabiliana na
janga la mafuriko kwenye maeneo ambayo hukumbwa na changamoto hiyo.
Aidha katika mkutano huo, Meya Mwita atatumia nafasi
yake kushawishi Umoja wa Mataifa, Mameya sambamba na Taasisi zinazo husika na
mabadiliko ya Tabia ya Nchi kusaidia changamoto za mafuriko ambazo zimekuwa
zikilikabili jiji la Dar es Salaam.
Meya Mwita alisema kuwa kupitia mkutano huo, wakazi wa
jiji la Dar es Salaam wategemee mabadiliko makubwa katika suala zima la utatuaji
wa changamoto ya mafuriko.
Hata hivyo baada ya kumaliza kwa mkutano huo atakunata
na kufanya mazungumzo na Meya wa jiji la Hamburg ambapo awali walikuwa na
makubaliano ya kuboresha miundombinu ya kuhifadhia takataka katika halmashauri
ya Kinondoni (Dampo).
No comments