Breaking News

Kauli ya Bavicha Geita kufatia kuripotiwa Wanachama 50 wa CHADEMA Kuhama Kumuunga Mkono Rais MAGUFULI

Image result for bendera ya chadema
NAKANUSHA HABARI YA WANACHADEMA 50 GEITA WAMEHAMA CHAMA KUMUUNGA MKONO DR MAGUFUlI.
Kuna Habari ambayo imeandikwa na mwandishi wa Habari wa Storm FM Bw Joel L Maduka katika Blog yake kuwa Wanachama wa chadema 50 wa kijiji cha Buligi Kata ya Senga Wilaya ya Geita wamehama kumuunga mkono Rais Magufuri kwa utendaji kazi.

Hii Habari ni ya uongo kabisa hakuna mwanachama yoyote aliohama kumuunga mkono Magufuri Bali wanamsubiria kwa hamu mwaka 2020 ili wamuadhibu kwa kutokumpa kura kwa sababu ya kuyafanya maisha yao kuwa magumu na kutokutimiza ahadi yake ya shilling mil 50 kila kijiji,

Hakuna mwanachadema Geita anaeweza kuhama kwa hiyali yake kwa kumuunga mkono Dr Magufuli kwani wanamfahamu vyema tokea akiwa Mbunge wa Chato ndio maana mwaka 2014 kwenye uchaguzi wa Serikali za mtaa jimbo la chato yeye akiwa Mbunge Chadema tulipata viti Vingi kuliko ccm.

Mimi nimuombe Rafiki yangu bw Maduka Maduka kuthibitisha kwa video na picha ambazo zinaonyesha hao wanachama 50 wa Chadema waliohama chama au aombe radhi kwa umma kwa kuandika Habari ya uongo la sivyo tutachukua hatua dhidi yake.

Niwaombe wandishi wa Habari wa Geita kwazingatia Sheria, Maaluma pamoja na miiko ya Taaluma zao ili kuondoa migongano sio ya Lazima.
Imetolewa na;-
Mhere Mwita,
M/kiti wa Bavicha (W) Geita,
Leo tarehe 10/11/2017.
Nakala kwa Makamu Mwenyekiti wa Club ya wandishi wa Habari mkoa wa Geita Bw Victor Bariety.

No comments