Taasisi Ya Elimu Ya Watu Wazima Yaendelea Kukuza Kwa Elimu Nchini
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha (kulia) akisisitiza jambo kwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt. Kassimu Nihuka wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt. Kassimu Nihuka,kushoto ni Mhadhiri wa Taasisi hiyo Dkt. Bernadeta Kapinga.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya watu Wazima
(TEWW) Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt. Kassimu Nihuka (katikati) akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William
Tate Ole Nasha (wakwanza kulia) kuhusu utendaji wa Taasisi hiyo ambapo
imepata mafanikio kwa kuongeza udahili kutoka wanafunzi 627 mwaka
2009/2010 hadi kufikia wanafunzi 3606 mwaka 2017/2018 kwa ngazi za
Astashahada, Stasgahada na Shahada, sawa na asilimia 575kutoka mikoa mbalimbali
ya Tanzania bara na Visiwani.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya watu Wazima
(TEWW) Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt. Kassimu Nihuka (katikati) akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William
Tate Ole Nasha kuhusu maktaba ya Taasisi hiyo wakati wa ziara yake katika
Taasisi hiyo mapema leo.
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)
wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha (Hayupo pichani) wakati wa ziara yake
katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha
akisisitiza jambo kwa kwa Viongozi wa Taasisi hiyo baada ya kupewa
maelezo kuhusu utekelezaji wa programu ya elimu masafa inayotolewa na Taasisi
hiyo mapema leo wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo. Picha na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).
Na
Samwel Gasuku- TEWW
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imetajwa kutoa mchango mkubwa
katika kukuza kiwango cha elimu hapa nchini kwa kuwa umuhimu wake unaonekana
katika jamii kupitia wataalamu wanaozalishwa na taasisi hiyo tangu kuanzishwa
kwake.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha amesema kuwa Taasisi
hiyo ni nguzo muhimu katika kuchochea ukuaji wa sekta hiyo kwa kuzingatia kuwa
inaendana na mahitaji ya sasa.
“Kwa sasa ni muda muafaka wa kuifanya Taasisi hii iweze kuwa mdhibiti
mkuu wa elimu ya watu wazima ikiwezekana hata tufanye maboresho ya sheria
iliyoinzisha TEWW ili kuipa nguvu ya kuwa mamlaka” Alisisitiza Waziri Ole Nasha
Akifafafanua Waziri Ole Nasha amesema kuwa ni wakati muafaka kwa Taasisi
hiyo kushirikiana na Taasisi mbalimbali katika kuimarisha utendaji na
kuongeza ubunifu ili kuwa na tija zaidi.
Aliongeza kuwa mfumo wa elimu ya Watu Wazima ni wa Kidunia hivyo ni vyema
kwa hapa nchini ukaendelezwa ili kuwapa fursa wale waliokosa katika mfumo rasmi
kujiendeleza na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi.
Pia alipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa hali
inayomsukuma kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo ili kupanua
zaidi wigo wa kutoa elimu yenye ubora unaoendana na mahitaji.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa TEWW Taaluma Utafiti na
Ushauri Dkt. Nihuka amesema kuwa tangu Taasisi hiyo ilipopata
ithibati imefanikiwa kuongeza udahili kutoka wanafunzi 627 mwaka
2009/2010 hadi kufikia wanafunzi 3606 mwaka 2017/2018 kwa ngazi za
Astashahada, Stashahada na Shahada, sawa na asilimia 575 kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.
”Taasisi yetu kwa kushirikiana na SIDO pamoja na Kiwohede kwa ufadhili wa
“ Commonwealth of Learning” imeanzisha programu ya kuzuia ndoa za utotoni kwa
wasichana wenye umri kati ya miaka 10-25 katika Mikoa ya Rukwa,Dodoma na Lindi
ambapo wasichana 3000 na wanajamii 10,000.” Alisisitiza
Akifafanua amesema juhudi za Serikali zimeiwezesha TEWW kununua vifaa kwa
ajili ya Kampasi ya WAMO morogoro na kukarabati kiwanda na ununuzi wa mitambo
mipya ya uchapaji itakayochochea na kuongeza tija katika Taasisi hiyo.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ilianzishwa chini ya Sheria ya
Bunge Na.12 ya mwaka 1975 na kupewa majukumu mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu ya
Watu Wazima kwa wataalamu,wawezeshaji na wasimamizi wa elimu ya Watu
Wazima nchini pamoja na kutoa mafunzo ya elimu ya kujiendeleza ngazi ya
sekondari nje ya mfumo rasmi kwa njia ujifunzaji huria masafa kwa vijana na
watu Wazima waliokosa elimu kwa sababu mbalimbali.
No comments