Washindi 10 wa Shindano La Vipaji Vya Sauti Wapatikana Sasa Kwenda China.
Washindi
wa Shindano linalodhaminiwa na kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia StarTimes
na chaneli yake ya Star Swahili lilifikia mwisho huku washindi 10 wakiibuka
kidedea katika mchakatio wa kuwasaka machampioni hao.
Miongoni
mwa watu walioibuka washindi ni Msanii wa filamu Bongo, Koletha Raymond,
aliyeibuka mshindi namba moja baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 25,
aliyokuwa akichuana nao kwa ajili ya kuwania nafasi ya kwenda kufanya kazi
makao makuu ya Kampuni ya Star Times, nchini China kuigiza sauti ya filamu
mbalimbali zilizochezwa kwa lugha mbalimbali.
Shindano
hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa LAPF lililopo
Millenium Tower Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo washindi 10,
wataungana na Koleta kwenda nchini humo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ambayo
wataifanya kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Washindi
hao wamepatikana katika ushindani mkali mbele ya majaji watatu wakiongozwa na
wasanii Jacob Steven ‘JB’ na Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambapo haikuwa kazi rahisi
kwa majaji hao na washiriki wenyewe kutokana na ushindani mkali uliojitokeza.
Washiriki
25, watano kutoka Mwanza, watano kutoka Zanzibar na 15 wa Dar es Salaam,
walichuana vikali kupata washindi 10 wanaokwenda kufanya kazi hiyo nchini China.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakifuatilia shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili kwa
mwaka 2017.
Makamu
wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka 2017 lililofanyika
katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Washindi
10 wa shindano la vipaji vya sauti walioshinda kwenda nchini China kufanya kazi
makao makuu ya Kampuni ya Startimes kwenye fainali hiyo iliyofanyika
katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa washindi walioingia kumi bora akipokea zawadi ya simu ya Startimes kutoka
kwa Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif mara baada ya
kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili lililofanyika katika
ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi(kulia)
akimkabidhi zawadi ya Television ya Startimes mshindi wa kwanza
wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili, Coletha Raymond mara baada
ya kuibuka mshindi wa shindano hilo
Mshindi
wa kwanza hadi wa tatu wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka
2017 wakiwa kwenye picha ya Pamoja.
Mshindi
wa kwanza hadi wa tatu wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili mwaka
2017 wakiwa kwenye picha ya Pamoja.
No comments