MAMA WEMA SEPETU AMTEMBELEA TUNDU LISSU NAIROBI
Mama Mzazi wa msanii wa filamu Bongo
na Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu wameenda Nairobi nchini Kenya
kumjulia hali mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu ambaye anapata
matibabu nchini huyo.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa akitibiwa Nairobi tangu
aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi September mwaka huu.
Viongozi mbali mbali wa kiserikali na
wa chama hicho wamekuwa wakienda kumjulia hali na sasa Mama wa Wema Sepetu
ameonekana kufanya hivyo.
Hapo jana Makamu wa Rais Mhe. Mama
Samia Suluu alimtembelea pia Lissu hospitalini hapo. Mama Wema pamoja na
mwanaye February 24 mwaka huu walitangaza kujiunga na Chadema
No comments