IGP SIRRO AZUNGUMZIA HALI YA UHALIFU KIBITI
MKUU wa jeshi la polisi nchini
(IGP)Simon Sirro amewahakikishia wananchi mkoani Pwani kuwa silaha zote
zilizochukuliwa na wahalifu wa ovyo ovyo huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote
mkononi mwa dola na kusambaratisha mtandao wa kiuhalifu.
Aidha ametoa rai kwa wazazi na walimu kutoa
taarifa kwenye vituo vya polisi mara watakapobaini kuna mwanafunzi mtoro ama
hajaripoti shule kwa miezi kadhaa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika
kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.
Pamoja na hayo IGP Sirro ,amesema vyombo vya
ulinzi na usalama nchini vinashirikiana na nchi ya Msumbiji kupambana na
wahalifu waliobainika kukimbilia nchini humo wakitokea Tanzania.
Aliyasema hayo wilayani Kibaha ,mkoani Pwani
,katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo pia alizungumza na viongozi wa
mashirika ya umma,wazee maarufu ,wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na
usalama mkoani hapo.
IGP Sirro alieleza kuwa ,vyombo vya ulinzi na
usalama vinaendelea kupambana na yeyote atakaekuja kwa moto nae wataenda nae
kwa moto na atakaekuja baridi wataenda nae baridi.
Alisema serikali imeshinda kwa hilo na hali kwa
sasa ni shwari katika wilaya hizo.
IGP Sirro alieleza amepatiwa taarifa ya
wanafunzi zaidi ya 1,300 mkoani hapo kuwa ni watoro na hawajulikani walipo
hivyo wazazi washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.
“Kuna baadhi misikiti,makanisa yanadaiwa
yanayotumia watoto hawa katika masuala ya kiuhalifu hivyo kuna kila sababu ya
kuingia ndani kutafuta suluhu “
“Ni kazi yetu wazazi jamii na walimu
kushirikiana ,na hapa ni muhimu wazazi wasaidie kusema watoto wao walipo ili
kuwa na usalama” alisema .
Katika hatua nyingine IGP Sirro alielezea
viongozi wa dini wana nafasi ya kuhakikisha wanatumia eneo lao kuhubiri amani .
“Tusidharau taarifa hata kama ni ndogo
,tusibweteke umoja ni nguvu tusaidiane kukomesha vitendo vya uvunjifu wa amani
” alifafanua IGP Sirro.
Akizungumzia changamoto ya wahamiaji haramu
alisema wanashirikiana na uhamiaji kuusaka mtandao unaohusika kufanya biashara
ya kusafirisha wahamiaji haramu .
IGP Sirro alisema hawatamvumilia yeyote
anaekumbatia wahamiaji haramu kwani ni chanzo cha kusababisha kuleta magaidi na
kusafirisha bidhaa za haramu .
Alisema kwasasa wamejipanga kutaifisha mali za
wafanyabiashara hao wa wahamiaji haramu na usafiri utaotumika kuwasafirisha.
Nae mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist
Ndikilo ,ameshukuru kuwepo Kwa kanda maalum kwani imeweza kuleta mafanikio
makubwa.
Alisema kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya
sintofahamu ,watu walisitiza shughuli zao za maendeleo ,biashara zilikwama,watu
na baadhi ya viongozi walihama nyumba zao na wengine kulala saa 12 jioni kwa
kuhofia mauaji.
Mhandisi Ndikilo alieleza sasa Kibiti na Rufiji
hali ni shwarii kutokana na kuimarishwa ulinzi.
Aliwataka pia wawekezaji na wadau mbalimbali
mkoani Pwani ,kujitokeza kushirikiana kusaidia kutatua changamoto zinazolikabili
jeshi la polisi ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ,usafiri na kujenga vituo vya
polisi .
Mhandisi Ndikilo, alisema kuwa Mkoa huo
umesheheni viwanda vya kutosha hivyo ni vyema kusaidia mambo hayo kwa manufaa
ya wote wakati kukitokea uhalifu.
“Tukikumbwa na uhalifu tunapigia simu polisi,
tusiwe Wa kwanza kulaumu wakati wa matatizo ,tukumbuke na kuwasaidia ili
kufanikisha kazi zao kifanisi.;:” alisema mkuu huyo wa mkoa .
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Pwani
,(ACP)Jonathan Shanna alisema ziara hiyo ni neema kwao na wamepewa maagizo
mbalimbali ambayo watayafanyia kazi.
Kamanda Shanna alisema wamemfikishia kero IGP
zinazowagusa askari polisi ikiwemo upungufu wa makazi .
No comments