Breaking News

DIWANI WA VIKINDU MHE NICHOLUS JOHN WAASA WANAFUNZI CHUO CHA WALIMU VIKINDU KUWA MAADILI KIPINDI CHOTE CHA MASOMO

 Diwani Wa Kata Hiyo Ya Vikindu Mhe Nicholus John .

Na Sala Mlawas-Dar
WITO umetolewa  kwa wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa kuwa na hekima pamoja na busara kwani wanapotoka vyuoni wanatarajiwa kwenda kuelimisha jamii na sio kupotosha .

Akizungumza na waandishi Wa habari Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti Wa Bodi Ya Chuo Cha Ualimu Cha Vikindu Na Pia Ni Diwani Wa Kata Hiyo Ya Vikindu Mhe Nicholus John  alisema ameamua kuwahamasisha wanafunzi Wa chuo hicho kuwa na maadili yanayostaili kwani wao wasipokua na maadili mazuri ni sawa na kwenda kupotosha jamii wanapotoka vyuoni.

“ Kitu ambacho kimenisukuma kutoa wito huu ni kufatia kuwepo kwa taarifa kuwa baadhi ya wanafunzi wanaotakiwa kufukuzwa chuo kutokana na kutokuwa na maadili mema ikiwemo vitendo vya utovu wa nizamu na uongo walivyokuwa wanafanya kwa walimu wao” Alisema John.
Diwani Wa Kata Hiyo Ya Vikindu Mhe Nicholus John akifafanua jambo katika mkutano wake na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Mhe john ametaja majina ya wanafunzi hao kuwa ni Husna Hemedi, na Zaituni Omary ambao walikua wamekidhiri kwa utovu wa nizamu na walimu kuchukua jukumu lakutaka kuwafukuza chuo.

Hata hivyo mhe John alisema ameamua kuwaombea msamaha ili wasiweze kufukuzwa kwani bado miezi mitatu waweze kufuzu masomo hayo na kwenda kutafuta ajira na pia aliona atawaumiza wazazi na walezi wao kwani wanafunzi wamekua wakilipiwa ada kwa wakati na wazazi  wakiwa na imani wanawasaidia watoto wao waje kujiendeleza katika maisha yao .
Aidha Mhe john aliongeza kuwa chuo hicho kimekuwa na changamoto mbalimbali zinazokikabili pamoja na ukosefu wa fensi , ukosefu wa ofisi za wakufunzi,  ukosefu wa uwanja kwa ajili ya mazoezi kwa vijana hao.

Pia Mhe John ameiomba serikali itenge fungu ambalo litaweza kutatatua changamoto hizo ikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu kwani wanatokea maeneo ya mbali inawadhalimu kuchelewa mda wa vipindi kwa ugumu wa usafiri.

No comments