UMASONI: WANAWAKE AMBAO NI FREEMASON NA ITIKADI ZAO
Wanawake wa
Freemason wamekuwa wakikongamana kwa zaidi ya miaka 100 sasa - wakifanya
matambiko na sherehe sawa na wenzao wa kiume.
Lakini si watu
wengi wanaofahamu kuwepo kwa kundi hili. Sasa tunaweza kukufahamisha zaidi
kuhusu shughuli za Freemason hawa wa kike baada ya kipindi cha redio cha
Victoria Derbyshire cha BBC kuruhusiwa kuzungumza nao.
"Freemason
ni nani?" anauliza mmoja wa viongozi wao ambao huitwa master (gunge)
katika Kongamano Tukufu la Jumuiya ya Freemason wa Kale.
"Ni mfumo
wa kipekee wa maadili ambao umezingirwa na istiari na ishara zenye maana,"
anajibu Dialazaza Nkela.
Nkela
anashiriki katika sherehe ya kipekee ya kumfikisha ngazi ambayo hufahamika kama
"shahada ya pili".
Ni sherehe ya
kusherehekea kupanda hadhi kwake katika kundi lake.
Kufikia kwake
"shahada ya kwanza" kuliadhimishwa kwa kuingizwa kwake katika kundi
hilo, shughuli ambayo ilihusisha yeye kuweka wazi "mkono wake wa kulia,
ziwa lake la kulia na goti la kulia" kitanzi kikiwa kimewekwa kwenye
shingo lake.
Kila sehemu ya
tambiko hilo, hudaiwa kuwa na maana yake - ingawa hatukufahamishwa zaidi.
"Shahada
ya tatu" hudaiwa kuwa "pale unapokumbana na kifo ili kuzaliwa
upya" na huwakilishwa na "mwisho wa uhai mmoja na kuanza kwa maisha
mengine".
Maana ya hili
pia, wanaweka siri.
Lakini
ufichuzi huu wenyewe ni kidokezo kuhusu shughuli na imani za kundi hili lenye
usiri mkuu.
Watu wengi
hata huwa hawafahamu kwamba kuna mafreemason wa kike.
Freemason wa
kiume - ambao walianza rasmi mikutano yao zaidi ya miaka 300 - wamekuwa
wakiangaziwa zaidi.
Kwa sasa
huongozwa na mwanamfalme mtawala wa Kent.
Lakini ukijumlisha makundi mawili yaliyopo ya
freemason wa kike - Honourable Fraternity of Ancient Freemasons na Order of
Women Freemasons, ambayo yaligawanyika mapema karne ya 20 - kuna
karibu mafreemason wa kike 5,000.
Wanachama wa
Order of Women Freemasons hukutana mara kwa mara katika mahekalu au nyumba kote
nchini Uingereza.
Wakati wa
sherehe zao, wanawake huvalia gauni ndefu za rangi nyeupe pamoja na mapambo
shingoni kuashiria cheo cha kila mwanachama.
Ibada zao
huanza kwa msafara kwenye njia kuu ya kuelekea kwenye madhabahu ndani ya
hekalu.
Wanachama wa
kundi hilo huinama wanapofika pale mbele, ambapo huwa ameketi mkuu wao ambaye
hufahamika kama grand master (gunge mkuu).
Grand master
(Gunge mkuu) wa sasa ni Zuzanka Penn ambaye huketi katika kiti kikuu ambacho
hufanana na kiti cha enzi.
Huwa kuna
maombi wakati wa ibada zao, na wakati mwingine unaweza kuhisi kana kwamba hilo
ni kundi la kidini, ingawa Bi Penn anasisitiza wkamba hilo si kundi la kidini.
"Ili uwe
wa Freemason, lazima uwe umeamini katika kiumbe (au roho) mkuu," anasema,
lakini unaweza kuwa katika "imani (dini) yoyote ile".
"Huwa
tuna watu ambao wana imani sana kidini, na wengine ambao hawafuati sana dini -
lakini ni watu wa asili mbalimbali, au imani mbalimbali," anasema.
Wengi wa
wanawake wamasoni huwa wana miaka 50 na kwenda juu - jambo ambalo wanataka sana
kubadilisha.
Kwa sasa,
wanawatafuta wanawake vijana, wakiwemo wale waliojiunga na vyuo karibuni, wawe
wanachama.
Mtaalamu wa
macho Roshni Patel anafanyiwa sherehe ya kumfanya kuwa wa ngazi ya Mastre
katika kundi hilo.
Alijiunga na
Freemason miaka saba iliyopita.
Hatukuruhusiwa
kuhudhuria sherehe hiyo, lakini tunafahamu kwamba alipewa "heshima"
ya kuketi kwenye kiti kile kinachofanana na kiti cha enzi.
"Shughuli
yote ya kuwekwa kwenye kiti hicho, ilikuwa ya kuteka hisia sana," anasema,
akiondoka.
"Hasa kwa
wanachama wote wa nyumba yetu, ambao wananidhamini sana."
Alipoulizwa
kuhusu kuwa Freemason wa ngazi ya master (gunge), aliongeza: "Bado nina
mshangao," huku akijaribu kukubali uhalisia wa ufanisi wake.
Lakini kikwazo
kikuu zaidi pengine kwa wale wanaotaka kujiunga na kundi hilo huwa ni sifa zake
za usiri mkuu pamoja na kuhusishwa kwake na ufisadi.
Kadhalika,
tuhuma kwamba wanachama wa kundi hilo hufaana na kusaidiana ili kufanikiwa
katika taaluma zao mbalimbali pamoja na biashara.
Hili si jambo
ambalo Bi Penn analitambua.
"Nimekuwa
wa Freemason kwa zaidi ya miaka 40 na sijawahi kuahidiwa chochote na mtu au
kumfaa mtu mwingine yeyote (kwa sababu ni wa Freemason).
"Huwa
unasikia hadithi hizi, lakini sijawahi kusikia kisa chochote kama hicho katika
Freemason kamwe."
Mwaka 1997,
kulikuwa na wito kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo Jack Straw
kwa maafisa wa serikali na majaji kufichua kwa hiari iwapo ni wanachama wa
Freemason.
Mpango huo
ulifutiliwa mbali baada ya Freemason kutishia kuishtaki serikali ya Uingereza.
Christine
Chapman, gunge mkuu (grand master) wa Honourable Fraternity of Ancient
Freemasons, anasema ingawa wana "maafisa kadha wa polisi (ambao ni
wanachama)...sijaona yeyote akisaidiwa [kwa sababu ya kuwa mwanachama]".
Lakini kwa
muda mrefu kumekuwa na tuhuma kwamba kundi hilo huhusika katika ulaji rushwa
katika idara ya polisi na idara ya mahakama.
Kanuni za
kimasoni husema wanachama wanafaa kusaidiana na kufaana na kuweka siri za
kisheria za wanachama wenzao. Hii imewafanya wengi kuwa na wasiwasi wa kutumiwa
wka kundi hilo kuendeleza ulaji rushwa.
Takwimu muhimu kuhusu Freemason
§
Kuna takriban wamasoni 4,700 wa kike
Uingereza, ukilinganisha na takriban wamasoni 200,000 wa kiume
§
Wafreemason hukutana katika hekalu ambalo pia
huwa wanaliita "lodge" (au nyumba). Inafahamika kwamba huko ndiko
waasi wa kale walikuwa wanakutana wakifanya kazi ya ujenzi wa kanisa
§
Huwa wanavalia aproni maalum za kimasoni,
utamaduni unaotokana na imani ya jadi kwamba wamasoni walitokana na waashi,
ambao walikuwa wanavalia aproni maalum kujilinda dhidi ya mawe wakifanya kazi
ya ujenzi
§
Ngazi ya "shahada ya tatu" huwa ni
ngazi ya mwisho katika kuwa mmasoni kamili. Sherehe ya kuingiza mtu katika
ngazi hii huhusisha kuhojiwa vikali, ambapo wazo la kumpa mtu "shahada ya
tatu" huwa na asili yake.
§
Mafreemason maarufu ni pamoja na Sir Winston
Churchill, Sir Arthur Conan Doyle, Rudyard Kipling, Robert Burns, Oscar Wilde
na Peter Sellers
Bi Chapman
anasisitiza kwamba usiri wa Freemason hutokana na haja ya kuunda mvuto fulani
na pia upekee fulani na si "kuficha uovu fulani".
"Hatuna
mipango ya kujaribu kutwaa udhibiti wa ulimwengu, licha ya dhana hizi ambazo
huenezwa na watu waongo mtandaoni, na hatujaribu kupindua serikali au mambo
kama hayo.
Moja ya mambo maarufu kuhusu umasoni huwa ni salamu zao - na kwa hilo hakuna tofauti kwa wanawake pia.
"Tunahitaji
kuhifadhi kiasi fulani cha usiri kwa sababi hilo ndilo hufanya kundi letu kuwa
maalum."
Ndio, bila shaka [tuna salamu zetu za
kipekee]," anasema Bi Penn, bila kueleza salamu hizo huwa vipi.
"Ni siri yetu. Ni lazima ujiunge
nasi kisha nitakwambia huwa zinahusu nini," anasema, huku akitabasamu.
Kuna mambo mengi watu huamini kuhusu
wamasoni, ikiwa ni pamoja na salamu zao za kipekee.
No comments