MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMJULIA HALI MH TUNDU LISSU JIJINI NAIROBI
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki
(Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Msafara wa Samia umefika hospitalini
hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk
Pindi Chana.
Mwananchi lililokuwapo hospitalini
hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini
hapo.
Lissu amelazwa hospitalini hapo
akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa
Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amefika hospitalini
akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa
kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza
wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa
Septemba 7.
No comments