Naibu Waziri Wa Afya Mhe Ndugulile Azindua Kampeni Ya Upimaji Macho, Shinikizo La Damu Na Kisukari Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Naibu
Waziri Wa Afya Mheshimiwa Faustine Ndugulile (Mb) leo amemuwakilisha Makamu Wa
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu katika
uzinduzi wa Kampeni Ya Upimaji Macho, Shinikizo La Damu Na Kisukari Mkoani
Pwani katika Wilayani Mkuranga.
Katika hatua hiyo Naibu Waziri Amempongeza
Mwenyekiti Wa Lions Club kwa jitihada anazofanya za kuunga mkono juhudi za
Serikali Ya Awamu Ya Tano kwa kampeni anayoendelea nayo ya huduma ya
upimaji wa afya bure katika jamii.
Aidha, Naibu Waziri Wa Afya ameeleza utafiti
uliofanywa na Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Shirika La Afya Duniani (WHO) na Taasisi Ya NIMR wa
Mwaka 2013, unaohusu Viashiria Vya Magonjwa Yasiyo Ya Kuambukiza,
umeonyesha Kuongezeka kwa viashiria hivyo, idadi ya Watanzania wenye
shinikizo la damu ni asilimia 25.9% na wagonjwa wa kisukari ni asilimia 9.1%.
"Hii Haikubaliki, ni lazima
tuongeze bidii katika kuyashughulikia magonjwa haya. Ni lazima Kwa pamoja
Serikali Na Sekta Binafsi tufanye kazi kwa bidii katika kupambana na
janga hili ambalo visababishi vyake vikubwa ni pamoja na ulaji usiofaa,
kutokufanya mazoezi, matumizi ya pombe na tumbaku kupita kiasi " alisema
Dkt Ndugulile.
Mheshimiwa Naibu Waziri amesema Serikali
inafanya kazi kwa kushirikiana na Wadau katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu
namna bora ya kujikinga na maradhi yasiyo ya kuambukiza kupitia njia
mbalimbali.
Katika hatua hiyo kliniki zipatazo 187 za
magonjwa yasiyo ya kuambukiza zimeanzishwa na kuimarishwa, kuanzia ngazi
Ya Vituo Vya Afya mpaka Hospitali Ya Taifa.
Aidha, Mheshimiwa Naibu Waziri alipata fursa
ya kutembea kiwanda cha KNAUF ambacho kinajishughulisha na uzalishaji wa Gypsum
Board Na Gypsum Plaster Na kuwapongeza kwa juhudi wanazofanya za kuunga mkono
Sera Ya Viwanda Nchini
Naibu Waziri aliwashukuru Uongozi mzima
wa Lions Club Dar Es Salaam kwa kushirikiana na Madaktari wa hospitali ya
Regency na Wilaya ya Mkuranga kwa kumualika na kuahidi Serikali Ya Awamu Ya
Tano itaendelea kuunga mkono juhudi zote wanazofanya na kuahidi kuwapa
ushirikiano wa karibu pindi watapohitaji.
No comments