Mhe Zitto Awataka Wachunguzi Wa Kimataifa Kuja Tanzania.
Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki
ya Dunia (WB) kufanya uchunguzi maalumu wa takwimu za kasi ya ukuaji wa
uchumi ya robo ya pili ya mwaka na kuchukua hatua endapo itabainika kile
anachodai kuwa Serikali ilipika takwimu.
Akuzungumza mapema leo jijini dare s salaam
kiongozi wa Act wazalendo Mhe Zitto Kabwe alisema chama hicho kimebaini kuwepo
sintofahamu juu ya takwimu zilizotolewa na Serikali za mwezi Aprili hadi Juni mwaka
huu kuwepo na mashaka juu ya Usahihi.
Alisema takwimu za Serikali zinaonyesha kasi
ya ukuaji wa uchumi katika robo ya pili ya mwaka ni asilimia 5.7, tofauti
na za ukokotozi kwa kanuni za kiuchumi anazodai zinaonyesha ni asilimia 0.1.
“Hatujatafuta takwimu nyingine, hizi ni
taarifa zilezile zilizotolewa na BoT na NBS lakini ukikokotoa utaona
uchumi tulionao unasinyaa badala ya kukua na hali ikiendelea hivi hadi
Juni 2018 kutakuwa hakuna uchumi Tanzania,” Alisema Mhe Zitto.
Alisema sababu hiyo inachangia maisha ya
Watanzania kuendelea kuwa magumu ilhali Serikali imekuwa ikitoa taarifa za
uchumi kukua.
Aidha mhe Zitto amegusia pia takwimu za
mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akidai nazo
haziko sahihi.
Amesema ni vyema wakati TRA ikitoa takwimu
zake ikaeleza mapato kwa kila idara bila kuchanganya marejesho na madeni
ambayo hayajalipwa.
“Taarifa yao ieleze kinagaubaga mapato ya
idara ya forodha, walipa kodi wakubwa na walipa kodi za ndani. Wasiishie
hapo, kati ya fedha wanazotaja kukusanya iwekwe wazi madeni na
marejesho ni yapi tofauti na inavyofanywa sasa,” amesema.
Zitto ametaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa mapato ya Serikali ya Julai na
Agosti na kuweka wazi taarifa hiyo.
No comments