LHRC Yaitaka Serikali Kufuta Sheria Ya Adhabu Ya Kifo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa LHRC Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupinga adhabu ya kifo leo jijini Dar es Salaam.
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) kimeitaka serikali kubadilisha sharia, kuondoa adhabu ya kifo kwa kuweka
adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na wafungwa waliopo katika vifungo vya
muda mrefu gerezani.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC
Anna Henga akizungumza na Mtandao wa Matukio360, amesema kuwa kituo hicho
kinaungana na Mtandao wa Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani katika maadhimisho ya
15 siku ya kupinga adhabu ya kifo.
Henga
amesema adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili ambayo inakinzana na misingi ya
utu na haki za binadamu kama ilivyoainishwa katika mikataba mbalimbali ya
kimataifa.
“Adhabu
ya kifo ni adhabu ya kikatili isiyo ya staha, inayotweza utu wa binadamu,
inafanya serikali ionekane pia kama mhalifu kwa kuua, tuitake serikali
ibadilishe sharia na kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye
makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vifungo vya mrefu,” amesema
Henga.
Aidha
LHRC kime mpongeza Rais John Magufuli kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutounga
mkono adhabu ya kifo kwani ni ya kinyama na isiyostahili binadamu yeyote.
Kwa
upande mwingine Henga ametoa sababu za kituo hicho kupinga adhabu hiyo.
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na adhabu kuwa ya kibaguzi kwani mara nyingi
wanaopatikana na hatia na kupewa adhabu hiyo ni maskini wasioweza kuwa na
ushauri wa kisheria na watu wengine.
Nyingine
ni vigumu kuthibitisha kuwa inatekelezwa tu kwa watu ambao wametenda na kukutwa
na hatia ya kosa hili au wabaya Zaidi, Adhabu hiyo ikitolewa kwa mtu asiye na
hatia kimakosa huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na
uwezekano wa kuwa na mianya ya makosa.
Ameongeza
nyingine kuwa ni adhabu kutompa nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya
kulipiza kisasi na wala haimsaidii mtu yeyote hata familia ya muathirika,
hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inazuia watu wengine kutokwenda makosa
kama hayo.
Pia
amesema sharia hiyo inamianya ya makosa na ni vigumu kuwa na uhakika kuwa haki
itatendeka kila wakati. Wapelelezi –ubambikiwaji wa kesi, changamoto za
kiupelelezi, waendesha mashtaka, huweza kufanya makosa, majaji kufungwa mikono
kulingana na uwakilishi mbele yao na kubanwa na sharia inayowataka kutoa adhabu
ya kifo kwenye makosa tajwa.
No comments