Breaking News

Muhimbili Kuanza Kutumia Kadi Katika Malipo

Muonekano wa card ya kufanya malipo iliyozinduliwa Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Lawrence Maseru Akizungumza katika uzinduzi Card mpya ya kulipia huduma za matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

Mkurugenzi mkuu wa MAXI COM AFRICA. Bw.JAMESON KASATI akifafanua jambo katika uzinduzi Card mpya ya kulipia huduma za matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa hospitali ya taifa ya Muhimbili Bw. Gerald Jeremiah.

Muonekano wa card ya kufanya malipo iliyozinduliwa jijini Dar es salaam.

Dar es salaam
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imezindua mfumo mpya wa kufanya malipo ya huduma kwa njia ya kielektroniki ambao utatupilia mbali malipo ya pesa taslim na malipo kuanza kufanywa kwa kutumia kadi maalumu au simu za mkononi.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Maseru mfumo huu unalenga kusimamia ukusanyaji mzuri wa mapato yanayotokana na malipo ya huduma hizo ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

“Mfumo huu pia utasaidia kupunguza adha kwa wagonjwa ya kufanya malipo kwa kukaa muda mrefu kwenye foleni ukizingatia hospitali hii inatoa huduma kwa watu zaidi ya elfu mbili kwa siku, hivyo mfumo huu mpya utapunguza adha wanazokabiliana nazo wagonjwa kila siku.” Alisema Profesa MUSERU.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa MAXI COM AFRICA Bw.JAMESON KASATI  alisema kampuni ya maxi com kwa kushirikiana na Hosptali ya taifa ya MUHIMBILI kwa pamoja wamezindua huduma  hiyo ya kieletroniki kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wagonjwa.

Alisema Maxi com Afrika imetengeneza mifumo kwa mitandao yote ya simu ambayo utatumika katika kulipia huduma za matibabu hospitalini hapo kulingana na aina ya mtandao husika kupitia menyu kuu ambapo mgonjwa atapata huduma hiyo.

Aidha Bw. KASATI aliongeza kuwa malipo yanaweza pia kufanyika kupitia card  maalum za hospitali ya taifa ya muhimbili pamoja na mitandao ya simu M PESA, TIGO PESA na AIRTEL MONEY.

No comments