Breaking News

Mhe Samia Wanawake Changamkieni Fursa Katika Majukwaa Ya Kiuchumi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo kwa kina mama (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya TTCL Kijitonyama.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Sophia Mjema akisisitiza jambo kwa kina mama (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa hilo iliyofanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akikata utepe wa mfano wa hundi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya TTCL Kijitonyama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu (kushoto) akipokea hundi toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama.
Baadhi ya kina mama wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi kwa Kinamama Mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama leo. (Picha zote na: Eliphace Marwa maelezo)

Dar ss Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan amezindua jukwaa la uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake wa mkoa wa dare s salaam sambamba na mfumo mpya wa utoaji wa huduma za kifedha wa benki ya CRDB ujulikanao kama “CRDB Bank SIMAccount” mfumo ambao unatarajiwa kutoa fusra kwa watanzania wengi kujiunga na mfumo rasmi wa kibenki kupitia simu za mkononi.

Akizungumza katika hafla hiyo mapema leo jijini dar es salaam Mhe samia amewataka wanawake kutumia jukwaa hilo kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli nyingne za kiuchumi.
“Nawaomba wakina mama tutumie Jukwaa hili kuongeza uelewa wetu katika upatikanaji wa mitaji, sheria za nchi katika masuala ya uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi kitu ambacho kitaswasaidia kujikwamua wao na familia na familia zao pamoja na taifa katika kupinga umaskini” Alisema Mhe Samia.

Katika hatua nyingine Mhwe samia ameipongeza benki ya CRDB kwa jitihada zake za kuhakikisha inakuwa benki ambayo inatoa huduma bora ikiwapo huduma mpya ya SIMAccount ambayo wamezindua leo hivyo kuwataka watanzia kujitokeza kwa wingikujiunga na huduma hiyo.

Alisema huduma ya SIMAccount itasaidia wananchi kufungua akaunti kupitia simu za mikononi hivyo kutoa rai kwa wakina mama wajasiliamali kujinga na mfumo huo kwani utawawezesha kujiwekea akiba kiurahisi kwa njia za vikundi ama binafsihivyo kwenda sambamba na sera ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda ambayo inasisitizwa na Rais Mhe John Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jukwaa la wanawake mkoa wa dar es salaam Mhe. Sophia Mjema alisema kupitia Jukwaa hilo ambalo kitaifa ni la 25 kuundwa wanawake wa mkoa wa dar es salaam watanufaika na fursa mbalimbali ambazo zitakuwa chachu ya kujikwamua kiuchumi pamoja na kutambua fursa mbali mbali zinazowazunguka.

Pia Mhe Mjema ametoa pongezi kwa wadau mbalimbali ambao wameshiriki kwa hali na mali kufanikisha uzinduzi huo ambapo ametoa pongezi kwa benki ya CRDB kwa kushirikiana kufanikisha siku hii muhumi kwa wanawake wa mkoa wa dar es salaam hii inadhilihisha jinsi ambayo benki hiyo inatambua mchango wa kina mama pamoja na kutoa kipaumbele kwa wanawake katika huduma zao. 

No comments