Kauli Ya Mhe Sumaye Kufatia Kunyang’anywa Mashamba Yake
Waziri
mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ametoa ufafanuzi kuhusu Rais Magufuli
kuchukua mashamba ya familia yake yaliyopo Dar es salaam na Morogoro.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo
Sumaye amesema chanzo cha migogoro hiyo ilianza mara baada ya kuondoka ccm na
kujiunga na upinzani ambapo tetesi zilivuma kuwa dawa ni kunyang'anywa
mashamba.
Sumaye amesema shamba la
Mabwepande lenye ukubwa wa heka 33 ambalo lilimilikiwa
kihalali na mtoto wake Frank Sumaye na lingine la mkewe Esta Sumaye lililopo
Mvomero lenye ukubwa wa heka 326 yamechukuliwa kwa visasi vya kisiasa.
Aidha amesema walifungua kesi tatu
ambapo mahakama ilitoa amri ya serikali kutoingilia mashamba hayo lakini jambo
hilo likapuuzwa.
Amehoji kuhusu agizo lililotolewa na
Waziri wa ardhi Lukuvi la kuendeleza shamba ndani ya siku 90 huko
Mabwepande eneo ambalo tayari lilishakaliwa na wavamizi ambao serikali
iliwalinda kupitia kauli ya mkuu wa wilaya ALLY HAPI kuwa wakae tu.
Amesema shamba la Mvomero tayari
liliendelelezwa na kwamba kuna visima viwili,umeme na mifugo na kutoa nukuu ya
jibu iliyowahi kutolewa bungeni kupitia wizara ya Ardhi kuwa shamba hilo
linatumika kihalali.
Sumaye amesema ni vema muhimili
wa utawala kuacha kuingilia muhimili wa bunge jambo ambalo hivi sasa polisi
wamekuwa wakiingia hadi bungeni na kusema haki ya mabavu siyo msingi wa
demokrasia.
No comments