Breaking News

Kauli ya Sheikh Ponda kufatia Maiti 15 Kukutwa katika viroba Ufukwe Wa Bahari.

Related image
Dar es Salaam.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amemwomba Rais John Magufuli kuwatoa hofu wananchi juu ya maiti 15 ziliookotwa zimefungwa kwenye viroba katika bahari ya Hindi.

Akizungumza jijini Dar es salaam alisema kitendo cha maiti hizo kuonekana zimefungwa kwenye viroba kinahatarisha maisha ya wavuvi wanaofanya shughuli zao katika bahari hiyo.

“Kitendo cha maiti 15 kuonekana zimefungwa kitaalamu na kuzitupie baharini tuna ninamwambomba Rais awatoe hofu wananchi na taifa kwani halijawahi kuleta  mauaji kama hayo,”alisema Ponda.

Alisema kwa mujibu wa taarifa zilizolipotiwa na  vyombo vya habari nchini kuokutwa maiti hizo baharini katika fuke za Tanzania bara na Zanzibar  zinaonesha kuwa wavuvi wanaofanya shughuli zao katika Baharini kusema mara nyingi wamekuwa wakiona na maiti za watu lakini wamekuwa na hofu kutoa taarifa Polisi.

Shekh Ponda aliongeza kuwa matukio kama hayo yanapotokea  lazima kuwepo na taarifa  itakayoonesha jitihada za serikali  ikishirikiana na Vyombo vya dola kuchukuliwa hatua za haraka kuchunguza tukio hilo na kutoa taarifa kwa wananchi juu ya wahusika wanaofanya matukio hayo.

“Sisi kama viongozi wa dini tunalaani mauaji ya kinyama kama haya katika taifa letu na sisi tunaamini nchi yetu ina amani  hii ni taarifa nzito,” Alisema Ponda.

Aidha shekh Ponda amezitaka Taasisi zinazojihusisha na maswala ya kutetea haki za binadamu kuongeza jitihada za katika kutambua Raia wanaishi katika mazingira gani ilikuweza kubaini matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana.

“Nitoe wito kwa Taasisi za haki za binadamu kuhakikisha zinatoa taarifa kwa wananchi juu ya kufatilizia maisha ya watu maiti 15 zinahitaji majibu ya kujua niakinanani wanaoteleza mauaji hayo,” alisema Ponda.

Pia shekh Ponda amewataka wananchi wote ambao ndugu zao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha lazima wahakikishe wanatoa taarifa sahihi kwa Jeshi la polisi  iliweze kufatilia tukio hilo kwa kuwasaka wote watakao husika.


“Wananchi msisite kutoa taarifa kwa Polisi  pamoja na Taasisi za kidini ilinasisi tuweze kulifatilia kwa uwezo wetu maana sisi kamwe hatukubaliani na mauaji ya watu ambao awana hatia” alisema Ponda

1 comment: