Huu Ndio Uamuzi Wa Mahakama Kuu Kwa Wabunge Wa Cuf Waliotumbuliwa Na Lipumba
Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajia kutoa uamuzi wa ama kuyasikiliza au
kutoyasikiliza maombi ya Wabunge 8 wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi CUF
waliofutiwa uanachama na Mwenyekiti Prof. Lipumba ifikapo August 4, 2017.
Hatua hiyo imetokana na Wakili
wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata kuwasilisha pingamizi la awali mbele ya Jaji
Lugano Mwandambo akipinga kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Malata ambaye anashirikiana na
Mawakili wengine Tisa alimueleza Jaji Mwandambo kuwa anapinga maombi hayo kwa
kuwa yamefunguliwa kwa njia isiyo sahihi akisema yamefunguliwa bila kuwekwa
kifungu sahihi kinachoipa Mahakama mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi dhidi
ya maombi hayo.
Aidha, amedai maombi hayo
yamefunguliwa chini ya kifungu kidogo cha 2(3) ambacho kinaipa mamlaka Mahakama
kutumia sheria ya Jumuiya ya Madola.
”Kama
maombi hayo yameletwa chini ya kifungu hicho ilipaswa kiwepo kifungu husika
kutoka katika sheria ya Jumuiya ya Madola, kisheria kinapaswa kutumika endapo
hakutakuwa na sheria yeyote Tanzania inayozungumzia maombi hayo”.Amesema Malata
Malata amedai maombi hayo ni
batili, hivyo yatupiliwe mbali kwani hata Mahakama iliwahi kutoa uamuzi dhidi
ya kifungu hicho.
No comments