Breaking News

Cuf Yatolea Ufafanuzi Uamuzi Wa Mahakama Kuu Juu Ya Kesi Ya Wabunge Nane Na Madiwani Wawili.

Chama cha Wananchi (CUF) kimeshangazwa na hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuendelea kumtambua Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba kwakuwa alijiuzuru kwa hiari yake na kutimkia nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Bw. Mbarala Maharagande, alisema kitendo hicho kinavunja na kukiuka Katiba ya chama hicho.

Alisema chama tayali kimefungua kesi kwaajili ya kutaka kujua ametumia vifungu gani kuendelea kumtambua Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa amejiuzuru kwa hiyali yake mwenyewe Sambamba wamefungua kesi nyingine dhidi ya Mwenyekiti huyo ya kuhoji uhalali wa kuwafukuza uanachama wabunge wanane na madiwani wawili wa chama hicho, kitu ambacho kimesababisha taharuki ndani ya chama.

Alisema kufatia kuvuliwa uanachama wabunge na madiwani na Lipumba walifungua shauri la msingi mahakama kuu (CIVIL CASE NO.143/2017) lakini pia kuna maombi madogo (Miscelleneous Civil Application No. 447/2017) ambayo inahusiana na kuomba Zuio la muda (Temporary Injuction Order and To maintain Status Quo)ambalo limeripotiwa ndivyo sivyo na kuleta sintofahamu kubwa kwa jamii pamoja na wanachama wa chama hicho.

Akitolea ufafanuzi shauri hilo Bw. Maharagande alisema Shauri la msingi (CIVIL CASE NO. 143/2017) Limepangwa kusikilizwa/kutajwa Tarehe 31/8/2017, ambapo kimsingi Wabunge na Madiwani wanadai haki ya uanachama wao kwa kuhoji mchakato uliotumika kufikia maamuzi hayo ambao haukufuata katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi yanayoendelea mahakamani.

Alisema wabunge hao Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za nidhamu dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa za tuhuma zao kwa maandishi ili waweze kujiandaa kwa utetezi, siku na tarehe ya kikao hicho ukizingatia kuwa si wote wanaoishi hapa Dar es Salaam.

Bw. Maharagande Aliongeza kuwa wameshtushwa na uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila kujiridhisha na wala kuwauliza na kujua kutoka kwao kilichojitokeza, kwa ujumla hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea.

Alisema kwa maamuzi huo tayali umekiuka katiba ya chama hicho kwa kushindwa kuzingatia haki za kikatiba ikiwemo kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5) ya katiba ya CUF, ambapo Wabunge hao tayali wamekatia Rufaa maamuzi huo na kuandikia barua na kukiomba Chama kupitia Katibu Mkuu kiweze kuitisha Mkutano Mkuu wa Taifa ili kufikisha rufaa yao.

“Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani ya Chama utolewa uhamuzi kama Lipumba na wenzake pale Baraza Kuu la uongozi taifa lilipowachukulia hatua za kinidhamu kwa kuwasimamisha uanachama Tarehe 28 Agosti, 2017” alisema Maharagande.

Kuhusu hatma ya shauri dogo ambalo limefunguliwa na wabunge nane na madiwani wawili ambalo lilitajwa tarehe 2 mwezi huu Bw. Maharagande alisema waliomba Mahakama Kuu itoe zuio la muda (Temporary Injuction Order and to maintain Status Quo) kusimamisha maamuzi ya bunge na tume na kuwarejesha wabunge waliovuliwa uanachama waendelee na shughuli za bunge na kuwawakilishi halali mpaka hapo shauri la msingi
litakapoamuriwa.

Alisema Kabla maombi hayo hayajasikilizwa Walalamikiwa (Respondent's No.1,2,3,4,5,8-15)waliweka Pingamizi la Awali (Preliminary Objections) juu ya shauri hilo kwa madai ya kukosa sifa za kisheria (incompetence enacted provisions of law) na hoja hizo 4 za pingamizi zilizosikilizwa takribani kwa masaa 4 Tarehe hiyo 2/8/2017 pale shauri hilo lilipoitwa kwa kusikilizwa na baadae kupangwa kutolewa maamuzi ya Pingamizi hilo jana Tarehe 4/8/2017.
“Pingamizi juu ya maombi ya Shauri namba 447/2017 yameondolewa mbele ya Mahakama na wala hakuna hiko kitu kinachoitwa ‘kesi imefutwa, au kutupiliwa mbali au mahakama imeruhusu Wabunge wapya kuapishwa, KWA HAKIKA HAKUNA USHINDI WA MAAMUZI YALIYOTOLEWA’ kama inavyoripotiwa” Aliongeza Bw. Maharagande.

Alisema Maamuzi hayo ya mahakama kuu yamewapa fursa ya kuandaa vizuri zaidi nyaraka hizo na tayari tumepata faida ya kujua hoja wanazosimamia walalamikiwa (Respondents) Wabunge tayari wameshaandaa nyaraka zilitayarishwa na kusainiwa zikiwa na marekebisho yote ya msingi na ya lazima yaliyopaswa kuingizwa ikiwemo kuwajumuisha katika shauri hilo Wakurugenzi wa Manispaa za Ubungo na Temeke ambao wanahusika kutokana na Madiwani waliopo katika halmashauri zao.

Aidha Bw, maharagande ametoa wito waandishi wa habari kuripoti habari za kimahakama kwa uashihi na kutumia weledi ili kuepusha taharuki na kuwachanganya wananchi na wadau na kuacha kuripoti taarifa kwa kutumia ‘ushabiki’ kwani mkanganyiko kwa kufanya hivyo haukujengi weledi na afya njema kwa kuwahabarisha wananchi ndivyo sivyo.

Pia amewataka wanachama wa CUF, Wapenzi na Watanzania kwa ujumla kupuuza habari za upotoshaji na propaganda kwani si shauri la msingi wala maombi ya zuio lililosikilizwa na Mahakama Kuu na kuyatolea maamuzi bali  Kilichotolewa maamuzi ni Pingamizi juu ya hoja za kisheria pekee ambazo zimesharekebishwa na kurejesha upya shauri hilo mahakamani.

No comments