TIB GROUP KATIKA MAONYESHO YA SABA SABA 2017
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgiic1VBI4YlltrVDyGKlK9B9PvFNoAiNT74-RLteP0QQjBcFhoRx64Tkmpb8IqVF7HCe2Qks_B0ljr5SOd38eFhTnAcSje2_t9N7JIu9JEKs4tR0eiCFgf87SdQIYETmp2gekJyY_EkjR/s640/SABA+7+TIB++2.jpeg)
Wafanyakazi wa TIB Group (TIB Development Bank Ltd, TIB
Corporate Bank na TIB Rasilimali Ltd) wakiwa tayari kutoa huduma kwenye
viwanja vya Maonyesho - Saba Saba.
TIB Group ina mashirika matatu yaliyoundwa
kimkakati ili kuiwezesha serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
ya nchi. Mashirika hayo ni
1. TIB
Development Bank Limited
2. TIB
Corporate Bank Limited
3. TIB
Rasilimali Limited
Pamoja na umoja huu, mashirika haya
yanajitegemea kiundeshaji na utendaji, kila moja likisimamiwa na
kuongozwa na dira na dhamira yake chini ya uongozi na bodi zao nazote zikiwa
chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
TIB Group tunakukaribisha
kutembelea banda letu la sabasaba ili upate elimu na taarifa mbali mbali kuhusu
huduma zetu.
Taasisi zetu zinatoa huduma mbalimbali za
kifedha ikiwamo ushauri katika masuala ya mitaji na uwekezaji,
mikopo ya miradi ya kimaendeleo na miundo mbinu pamoja na huduma mbalimbali za
kibenki za biashara.
UWEZO TUNAO......Tumejipanga
kutoa huduma mbali mbali za kifedha ili kusaidia ukuwaji wa biashara katika
kuwezesha maendeleo ya viwanda.
TIB Development Bank Ltd (TIB DFI) ni Benki ya maendeleo inayojihusisha na kutoa mikopo mbali mbali ya muda wa kati na muda mrefu. Mikopo hii inalenga sekta muhimu zinazochochea maendeleo ya nchi.
Sekta hizo ni pamoja na miundo mbinu, uanzishwaji na uundwaji wa viwanda mbalimbali, miradi ya Gesi, ufuaji wa madini, miradi ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo na miradi ya huduma za kijamii.
Uzoefu wa benki hii katika kuwezesha maeneo haya una msingi imara kutoka kuanzishwa kwa Taasisi hii mwaka 1970.
Kwa mawasiliano zaidi:www.tib.co.tz
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjD0wWPLMCc9cQYBA_6w5R4rczEVqsQf60Cp-bIU2qsLOxWLMdtv72ibBX-ARiu-xzNafG-rfu34c9mVUV4TaA1aYz4O9HJnQ8cDE8L8pZXN5XHrXJ8gq_1sBxNg7o_MkgH0LwQKxX1AI5S/s640/SABA+7+TIB+1.jpg)
Mkurugeni mtendaji wa kampuni ya Global Packaging
Ndg Joseph Wasonga(wa pili kulia) akiwapa maelezo wakurugenzi wa TIB juu
ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo. Wa kwanza kushoto ndugu Frank
Nyabundege Mkurugenzi mkuu wa wa TIB Corporate Bank . Wa pili kushoto
Charles Singili –Mkurugenzi Mkuu wa TIB Development Bank na wa mwisho kulia ni
Bi Theresia Soka mkuu wa kitengo cha masoko – TIB Corporate Bank Ltd. Kiwanda
cha Global Packaging ni miongoni mwa wateja ambao wamenufaika na mikopo
inayotolewa na benki ya TIB. Kiwanda hiki ni miongoni mwa viwanda vya kisasa
ambavyo vinazalisha vifungashio mbali mbali
TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya biashara
inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za kibenki za
kibishara kwa mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali
na binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.
Benki ina matawi 6 kwa sasa,
Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya.
Benki inatoa huduma mbalimbali
kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na;
akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali
mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na
ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati
fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja
na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka
Huduma zote hizi hutolewa kwa umahiri na
ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki. Pia
huduma ya ‘Premier Banking’ kwa wale wateja wanaopenda huduma maalumu na
kujitofautisha zaidi. Kwa mawasiliano zaidi:www.tib.co.tz
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXBGCg134yU6C21HTI61mO1_u0gzRPlganAIXf8yDx5nQc1pPwP-Y_qtahI6wFym1ygRHyAkHxqS-smYs8P-5ELDhIc7QpwM6VVMgtSoqbi315BvHbfpIX_LBVhyphenhyphenQKmNZcOI9i717tmnAJ/s640/SABA+7+TIB+3.jpg)
Wafanya kazi wa TIB Corporate Bank Ltd katika picha ya
pamoja, wakiwa tayali kuwahudumia wananchi mbalimbali watakao tembelea
banda lao katika Viwanja vya maonyesho saba saba.
TIB Rasilimali Ltd ni taasisi ya tatu katika muundo huu wa
TIB Group inayojihusisha na masuala ya uwekezaji katika masoko ya mitaji kama
vile ununuaji na uuzaji wa hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la
hisa Dar es salaam (DSE). Pia kutoa ushauri wa kifedha na kuwezesha utafutaji
wa mitaji.
TIB Rasilimali ndio wakala pekee wa soko
la hisa la Dar Es salaam inayomilikiwa na serikali. Imesajiliwa na mamlaka ya
masoko ya mitaji na dhamana(CMSA),pia inajihusisha na masuala ya usimamizi wa
fedha (fund management) chini ya usajili wa Mamlaka ya usimamizi wa mifuko ya
jamii (SSRA).Kwa mawasiliano zaidi:invest@rasilimali.tib.co.tz.
No comments