MBUNGE JULIANA SHONZA AANZISHA TIMBWILI, NUSURA APIGWE
Hali ilivyokuwa mapema leo katika viwanja vya bunge mara baada
ya kuibuka mzozo kati ya MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza na kunusurika
kupigwa na wabunge wa upinzani.
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza, amezua timbwili nje
ya viwanja vya bunge na kunusurika kupigwa na wabunge wa upinzani kutokana na
kuwatambia kwamba atahakikisha Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye yuko
kifungoni anaendelea kusota huko.
Katika
kauli yake Shonza ambaye aliongozana na Mbunge wa Viti Maalum wa CCM, Rose
Tweve alizungumza akidai ataleta maoni bungeni ili Mdee aendelee kusota nje ya
bunge kutokana na alichodai matendo yake anayofanya hayaendani na hadhi ya
kibunge.
Bila kutarajia Shonza alikutana na jibu la Mbunge wa Mlimba,
Suzan Kiwanga (Chadema) ambaye alikuwa pembeni akimtaka kuacha roho mbaya na
kumuogopa Mungu kwani hata Mdee akikaa nje ya bunge hatofaidika na jambo
lolote.
"Acha roho mbaya wewe ni mwanamke unafurahia vipi mwenzako
akipata matatizo? kukaa kwake nje hakuwezi kukusaidia kitu ila malipo ni hapa
hapa duniani "alisema Kiwanga kauli iliyoonesha kumkera Shonza hivyo
kuamsha timwili
Shonza alianza kujibu ndipo baadhi ya wabunge wa Chadema
waliokuwa jirani akiwemo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, Mbunge wa Babati Mjini,
Pauline Gekule, wakaanza kumtaka awe hekima kwa kuangalia umri wa mbunge
aliyekuwa akimtolea maneno machafu.
Hata hivyo Shonza hakutaka kuelewa na badala yake aliendelea
kuzungumza huku akilia ndipo Tweve na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Zainab Vullu
wakamvuta kumtoa nje ya geti la bunge huku yeye akiwataka wamuache .
"Niacheni kama wanataka kunipiga tuone, niacheni niacheni,
"alizungunza Shonza huku akijivuta kutoka mikononi mwa waliokuwa wanambeba
Wabunge wa Chadema waliwasihi kina mama wa CCM kumfunza Shonza
adabu ili ajue kuheshimu watu anaozungunza nao na apunguze jazba sio kutaka
kugombana na watu wazima.
"Mheshimiwa Vullu mfunzeni adabu huyu binti ana matatizo
makubwa haiwezekani anajibishana na watu wazima huku akitaka kupigana nao, ni
aibu mnatuambia sisi tuambizane ukweli lakini huyu binti mnamuangalia
anaharibikiwa "alisema Gekule
Mbunge wa Viti Maalum Upendo Peneza ambaye alikuwepo eneo la
tukio alisema "Tatizo la Shonza ana mtindo wa kukurupuka na anafanya mambo
bila kufikiria na amejitia aibu kutaka kupigana na watu wazima, nakumbuka mimi
alishawahi kunichongea bungeni kuwa nimevaa nguo mbaya isiyoruhusiwa wakati
siku hiyo hakuwa amekutana na mimi nilivyonyanyuka akashikwa na aibu mwenyewe
kwani nguo yangu ilikuwa sawa "
Wabunge waliokuwa wanashikiliwa wameachiwa na wametakiwa waripoti Polisi kesho asubuhi
Wabunge waliokamatwa ni;
Mhe Saed Kubenea.
Mhe Fanc Mwakajoka
Mhe Sesilia Pareso
Mhe Pauline Gekuk
Mhe Cecil Mwambe
Mh Devota Minja hajakamatwa ila anatafutwa na Polisi.
Mhe Saed Kubenea.
Mhe Fanc Mwakajoka
Mhe Sesilia Pareso
Mhe Pauline Gekuk
Mhe Cecil Mwambe
Mh Devota Minja hajakamatwa ila anatafutwa na Polisi.
No comments