MEYA ISAYA MWITA:WATANZANIA TUJIEPUSHE NA TABIA YA KUBAGUANA KIITIKADI ZA VYAMA, DINI NA KABILA BAADALA YAKE WAENDELEZE UMOJA, UPENDO NA MSHIKAMANO.
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita amesema Watanzania wanapaswa kujiepusha na tabia ya
kubaguana kiitikadi za vyama, dini na kabila baadala yake waendeleze umoja,
upendo na mshikamano.
Mwita, alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee ya
kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of God
(TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini.
Alisema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kubain mambo
mbalimbali ambayo yameanza kujitokeza nchi ambapo
kama Watanzania, watashirikiana na viongozi wa dini katika kusimama na
kuliombea Taifa anaamini viashiria vyote vyenye kuashiria vunjifu wa sheria
vitatoweka na nchi ikibaki kuendelea na umoja na mshikamano.
"Tangu nimezaliwa sijawahi
kushuhudia vita, machafuko katika nchi yetu, kikubwa huwa naona amani
iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa nawasishi sana ndugu zangu tuendelee kuwa
wamoja tusibaguane, kwa namna yoyote ile , ili nchi yetu iendelee kuwa na
amani.
"Baba wataifa
Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake alikuwa akisisitiza sana
kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo hai hadi sasa , mambo ya vyama,
Udini, Ukabila tuweke pembeni tusimame kama Taifa moja,"alisema Mwita.
Awali akijibu risala
iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Mwita aliahidi kuchangia katika ujenzi
huo mifuko 100 ya saruji na kiasi cha fedha sh 500,000 huku akiwataka waumini wa
kanisa hilo kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.
Katika risala hiyo,
ilieleza kuwa sh. Mil. 95 zinahitaji katika kukamilisha ujenzi wa kanisa la
kisasa ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 600.
No comments