TAARIFA KWA UMMA KUTOKA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA
Idara ya Uhamiaji inapenda
kuwakumbusha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni
wote kuhakikisha wamehakiki vibali vyao kupitia Mfumo wa Uhakiki ambao
unapatikana kupitia Tovuti ya Idara ya www.immigration.go.tz kabla ya zoezi la uhakiki
kuisha tarehe 19/07/2017.
Kwa wale ambao kumbukumbu za vibali
vyao hazitaonekana katika mfumo wa uhakiki au kuwa na tatizo lolote
wanashauriwa kuripoti katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa au kwa Mamlaka husika
ndani ya muda uliotolewa.
Baada ya kuisha kwa muda uliotolewa,
Idara itafanya ukaguzi nchi nzima na kuwachukulia hatua za kisheria Wageni
binafsi, Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo wageni
wao watabainika kuwa na vibali vya kughushi au vilivyopatikana nje ya utaratibu
wa utoaji vibali.
Idara ya Uhamiaji ilitoa muda wa siku
90 kwa wale wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki vibali vyao; tangu tarehe ya
kuzindua mfumo huo tarehe 19 Aprili, 2017.
Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
No comments