CHAMA CHA ADC CHAMWOMBA RAIS KUONDOA KATAZO LA KUTOFANYA MIKUTANO YA KISIASA NA KUTOA NENO KWA CHADEMA KUACHA KUINGILIA MGOGORO WA CUF.
Katibu mkuu wa chama
cha ADC-Dira ya Mabadiliko Bw. Doyo Hassan Doyo akiongea katika mkutano na
waandishi wa habari, pembeni yake ni Naibu katibu mkuu Bi. Queen Sendiga.
Dar es salaam.
Chama cha alliance
for democratic change (ADC), Dira ya Mabadiliko kimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuondoa katazo kwa vyama vya siasa nchini
kutofanya mikutano ya kisiasa na makongamano kwani vyama hivyo vipo kwa mujibu
wa sheria za nchi.
Akizungumza jijini
Dar es salaam kuelekea kilele cha miaka mitano tangu kuanzishwa katibu mkuu wa
chama cha Hicho Bw, Doyo Hassan Doyo alisema katazo hilo la kutofanya mikutano
ya kisiasa nchini limekuwa na athari sana kwa vyama vichanga ambavyo havina
wabunge, madiwani na wenyeviti wa
serikali za mitaa.
Alisema chama cha ADC
kimwomba mhe Rais Magufuli kuondoa katazo hilo kwani ni haki ya chama cha siasa
kwa mujibu wa sheria kuendesha shughuli zake kwa njia ya mikutano ambapo
wamekuwa wanadi sera za vyama vyao kwa wananchi.
“katazo la kuzuia
kufanya mikutano kwa vyama vya siasa na kutoa nafasi kwa wabunge na madiwani
ambao wamechaguliwa kuendesha mikutano katika maeneo yao ni kuvidhoofisha vyama
vichanga ambavyo havina wabunge, madiwani na viongozi wa serikali za mitaa”
Alisema Bw. Doyo.
Akiongelea mgogoro
unaoendelea ndani ya chama cha wananchi CUF kati ya mwenyekiti anayetambuliwa
na msajili Prof Lipumba na katibu mkuu wake Maalim Seif ameshauri viongozi hao
kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao.
Alisema kushindwa kupatia
ufumbuzi wa haraka mgogoro huo jambo hilo litapelekea wanachama wao kukata tamaa
hivyo kutishia Uhai wa chama hicho pamoja na kuviathili vyama vingine vya
upinzani nchini.
Aidha Bw. Doyo ametoa
onyo kwa chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA) kuacha mara moja kuingilia
mgogoro unaoendelea ndani ya CUF kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha
uvunjifu wa amani pia ni kukiuka sheria na taratibu za vyama vya sasa.
Pia chama cha ADC
kimempongeza Rais magufuli kwa hatua ambazo amekuwa akizichukua kuhakikisha analinda
asilimali za nchi hususani madini pamoja na bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
kwa kupitisha sheria mpya ya madini ambayo itasaidia kupunguza ubathilifu wa asilimali
hiyo ya taifa.
Katika hatua nyIngine
chama cha hicho kimelaani mauaji ya raia yanayoendelea kuripotiwa mkoani Pwani
na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo vya ulinzi na
usalama hili wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua za kisheria kwani jambo
hilo ni la kitaifa sio chama kimoja cha siasa.
Chama cha ADC dira ya
mabadiliko kinatajia kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake ambapo chama
kitaadhimisha kwa kufungua matawi, kutembelea wanachama wake pamoja na taasisi
mbalimbali.
No comments