RAIS MAGUFULI KUFUNGA MIGODI
RAIS
wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ametishia kufunga migodi yote inayomilikiwa
na makampuni ya nje ikiwa makampuni hayo yatasshindwa kuanzisha mazungumzo
haraka juu ya umiliki wao pamoja na tozo wanazopaswa kulipa.
Rais
Magufuli ameyasema hay oleo katika mkutano wa hadhara katika wilaya ya Kakonko
mkoani Kigoma ambapo yupo kwa ziara ya siku tatu. Amesema haiwezekani makampuni
hayo yanaendelea kuwa kimya wakati wameshakubaliana kuanzisha mazungumzo
haraka.
"Makampuni
ya madini yaliyoahidi kukaa na serikali kuzungumza, wafanye haraka wakiendelea
kuchelewa nitafunga migodi yote wanayomiliki" Rais Dk John Pombe Magufuli,
leo Kakonko, Kigoma.
Katika
Mkutano huo Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kigoma na
Watanzania kwa ujumla kuwa ataendelea kupambana na kodi zenye kuwakera wananchi
hasa wananchi wa hali ya chini.
Amesema
mpaka sasa serikali imeondoa kodi katika kilimo na mazao takribani 80 ambazo
zilikuwa kero kwa wakulima na itaendelea kuzipunguza mpaka wakulima wafaidike
na kilimo hicho.
“Tumefuta
tozo 80 katika kilimo na mazao. Tushikamane wakulima wote ili kuendeleza nchi
yetu, na tumefuta tozo zaidi ya 50 katika mifugo na bado tutaendelea kuzifuta
tozo kwa wananchi wanyonge ili wafaidike na kilimo pamoja na ufugaji” amesema
Rais Magufuli.
Kwa
muda mrefu wakulima vijijini wamekuwa wakipata usumbufu wakati wa kusafirisha
na kuuza mazao yao kwa kubambikiwa kodi nyingi. Hali hii inawarudisha nyuma
wakulima badala ya kufaidika wanazidi kuwa masikini kwa kupoteza nguvu nyingi
lakini hakuna wanachokipata.
Tangazo
hilo toka kwa Rais wao limekuwa faraja na mkombozi mkubwa kwa wakulima wengi
pamoja na wafugaji ambao Rais Magufuli amesema imefikia wafugaji walikuwa
wanalipa kodi ya kwato kwa maana ya kila kwato ilikuwa ikilipiwa kodi.
Akiwa
njiani kutoka Wilayani Kibondo kuelekea Wilaya ya Kasulu, Rais Magufuli
alilazimika kusimama njiani kuzungumza na wananchi waliojazana kutaka
kumsikiliza. Aliwaambia kuwa maamuzi aliyoyafikia naa kutangaza jana kuwa wakimbizi
warudi nyumbani kwao kwa kuwa kuna amani sio kwamba anawafukuza bali ni ukweli
kuwa wakimbizi wanachukua asilimia kubwa ya bajeti ya serikali katika mkoa huo.
“Kuna
wakati wakimbizi katika mkoa wa Kigoma walikuwa wengi kuliko wananchi wa mkoa wa
Kigoma. Huduma za maendeleo zilikuwa zikitumika kwa wakimbizi kuliko wananchi
walengwa. Sasa Burundi ni shwari wakimbizi warudi kwao wakalime wale kwa jasho
lao" amesema Rais Magufuli.
Akaongeza
kuwa yeye hakuchaguliwa na Watanzania kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi wa
Burundi bali amechaguliwa na mamilioni ya watanzania kwa ajili ya kuwaletea
maendeleo watanzania na nchi yao kwa ujumla.
"Nilichaguliwa
kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania sio kwa maendeleo ya wakimbizi" Rais
Dk John Pombe Magufuli akiwa njiani Wilayani Kibondo kuelekea Wilayani Kasulu
Mkoani Kigoma
No comments