Breaking News

WANAWAKE WEKENI MKAZO KATIKA MALEZI BORA ILI KUWA NA TAIFA BORA NA LENYE MAADILI.

Wito umetolewa kwa Watanzania kulinda amani tuliyonayo na kudumisha maadili katika jamii ili kuwa na Taifa bora na lenye maendeleo.

Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa kongamano kubwa la siku tatu la kuombea Taifa Naibu waziri Elimu, sayansi, Tekinolojia na Ufundi Injinia Stella Manyanya alisema wananwake ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha wanatilia mkazo katika swala la malezi bora jambo litakalopelekea taifa linakuwa bora.
Alisema hili kuwa na kuwa na taifa bora na lenye maendeleo chanya mkazo zaidi unaitajika kwa walezi kwa kuwalea vijana katika misingi bora ni jukumu la wanawake hivyo kupitia kongamano hilo litawasasaidia kuwajegea uwelewa washirki kutambua wajibu wao katika familia.
Aidha amewataka watanzania kumuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dk.John Pombe Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano kwa hatua anazochukua kuleta maendeleo sambamba na kupigania haki za wanyonge na masikini.
Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano la wanawake waombolezao kwajili ya  Taifa Mchungaji Deborah Godfrey Malassy alisema watanzania tuna kila sababu ya kujivunia kumpata Rais muadilifu, mchapakazi na mwenye kupigania rasilimalia za nchi ambazo zimekuwa zikipotea na kukosesha haki za wanyonge hapa nchini.
Alisema rais Magufuli ni tunu kwa taifa kwani taifa limekuwa likipoteza asilimali zake lakini kwa hatua ambazo ameanza chukua rais Magufuli inaonyeshakuzaa matunda hivyo kuwataka watanzania wote kila mmoja kwa imani yake kumwombea rais hili aendelee kutekeleza majukumu yake.
Nae  Mchungaji Emanuela Mtafikilo akiwasilisha mada katika kongamano hilo alisema jukumu la kila mzazi kulinda maadili kwa watoto na kutenga muda wa  kukaa na watoto wao hili kujua tabia za watoto kwani jambo hilo linajenga upendo.
Alisema kumekuwa  na tabia za wazazi kuwaachia watoto wakitumia mitandao ya kijamii na kuangalia vipindi vya luninga wakati wote jambo ambalo linapelekea kuwepo  mmomonyoko kubwa wa kimaadili.

No comments