CAF YATANGAZA MABADILIKO YA TAREHE KOMBE LA MATAIFA BINGWA AFRIKA
Kombe
la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai shirikisho la
soka barani Afrika limethibitisha.
Mchuano huo huwa unafanyika mnamo mwezi Januari na Februari na
kusababisha migogro na vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji
katikati ya msimu.
Kinyang’anyiro hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon
kitashirikisha timu 24 badala ya 16.
Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF katika
mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.
Michuano hiyo imekuwa ikishirikisha timu 16 tangu 1996.
Upanuzi wa mechi hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon
ambayo itaanda fainali ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya
kati akilazimika kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.
Mashindano hayo yataendelea kila baada ya miaka miwili barani
Afrika.
Caf ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu mataifa kutoka mabara
mengine kushiriki ama hata kuandaa mchuano huo.
Tangazo hilo kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na rais
wa Caf kuzungumzia hali ya soka barani Afrika..
No comments