MHE SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA.
Skauti mkuu Bi. Mwantum Bakari Mahiza
akifafanua jambo pembeni yake ni eline Kitaty Kamishna Mtendaji wa chama cha
skauti Tanzania.
Dar es salaam
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha miaka 100 ya tangu kuanzishwa skauti
Tanzania ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 29 Julai mwaka 2017 mkoani
Dodoma katika ukumbi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam Skauti mkuu Bi. Mwantum Bakari Mahiza alisema ufunguzi wa
maadhimisho hayo ambayo yatafunguliwa rasmi tarehe 26 mwezi huu yatawakutanisha
skauti zaidi ya elfu nne kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
ALisema pia washriki ktoka katika
nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemocrasia ya kongo
na kutoka nchi zingne barani afrika, Asia na Ulaya utajadili mambo mbalimbali
ikiwemo changamoto wanazokutana nazo katika kipindi cha miaka 100.
Aidha Bi mahiza aliongeza kuwa maadhimisho
hayo yatahitimishwa kwa kufungwa siku ya tarehe 28 mwezi huu na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
Maadhimisho hayo yamepewa Kauli mbiu
ya maadhimisho ya skauti ni "Kuwajenga Vijana kuwa Wazalendo na Kufanya
Kazi kwa Bidii kwa Maendeleo ya Nchi"
Chama cha Skauti kilianzishwa mwaka
1905 na badae huko Uingereza na muasisi Lord Baden-Powell na baadae kiliingia
Zanzibar na hatimae Tanganyika mwaka1917.
No comments