HUU NDO UHAMUZI WA MAHAKAMA KUFATIA RUFAA YA SERIKALI DHIDI YA VIONGOZI UAMSHO.
Kutokana na hali hiyo, mahakama hiyo ya Rufani imefuta mwenendo
wa Mahakama Kuu kuhusu maombi ya marejeo yaliyokuwa yamewasilishwa na viongozi
hao wa Uamsho na kuelekeza shauri liendelee katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu pale lilipofikia kabla ya maombi hayo kupelekwa Mahakama Kuu.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na jopo la majaji watatu likiongozwa
na Jaji Batueli Mmila, Rehema Mkuye na Kipenka Mussa. Jopo hilo lilifikia kutoa
hukumu hiyo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili pamoja na sheria zilizoainishwa
ambazo ni Kifungu namba 243 na 246 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai,
kwamba hakuna ubishi kuwa mamlaka ya mahakama ya chini yana mipaka.
Jopo hilo limesema mamlaka ya hakimu ni madogo ambayo
anaruhusiwa kuamuru hati ya mashitaka kusomwa kwa washitakiwa na kusomwa kwa
hati za mashahidi ambapo baadaye wanapeleka shauri hilo mahakama kuu kwa ajili
ya kusikilizwa.
Kwa sheria hiyo, hakimu hana kazi nyingine zaidi ya kuruhusu
hati kusomwa kwa washitakiwa kwa hivyo, masuala yaliyoainishwa Septemba 3, 2014
yalikuwa ni masuala ambayo mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka na kwamba
yalitakiwa kusubiri kuzungumzwa mara baada ya kupelekwa mahakama Kuu
kusikilizwa.
“Tumekubaliana na upande wa mashitaka ukiongozwa na Peter Njika
kwamba pale ambapo mahakama ingeona kuna mapungufu kwenye hati ya mashitaka,
Hakimu anachopaswa kufanya ni kushauri upande wa mashitaka kuondoa mashauri
hayo,” lilisema jopo hilo, na kuongeza kuwa haikuwa sahihi kwa Jaji Dk Fauz
Twaibu wa Mahakama Kuu kuleta tafsiri kwa kujumuisha hata makosa
yanayosikilizwa na Mahakama Kuu.
Serikali iliwasilisha rufaa hiyo dhidi ya walalamikiwa kupinga
uamuzi wa Mahakama Kuu wa Desemba 19, 2014. Mbali na Ahmed, washitakiwa wengine
ni Jamal Swalehe, Nassor Abdallah, Hassan Suleimani, Antari Ahmed, Mohammed
Yussuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally, Juma Sadala Juma, Said Ally, Hamis
Salum, Said Salum, Aboubakar Mngodo, Salum Ally Salum, Salum Armor Salum, Alawi
Amir, Rashid Ali Nyange, Amir Juma, Kassim Nassoro, Said Sharifu, Mselem Mselem
na Abdallah All. Julai, 2014, Ahmed na wenzake 21 walipandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka matatu ya
kula njama kutenda kosa, kusajili watu kujihusisha na ugaidi na kuhifadhi watu
wanaojihusisha na vitendo vya ugaidi.
No comments