Breaking News

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA HISA ZA KAMPUNI YA JATU PLC HILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa JATU Plc Bw. PETER ISARE GASAYA akifafanua jambo

kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini (JATU PLC) imejikita katika kutoa elimu juu ya mikopo, kilimo na masoko kwa wananchi hili kuwawezesha kutokomeza umaskini kwa kutumia Rasilimali watu, kilimo na Viwanda.

Akizungumza katika banda lao katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere Sabasaba Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa JATU Plc Bw. PETER ISARE GASAYA alisema kampuni hiyo ya Umma ilianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha wakulima na kuwapa elimu kuwawezesha kulima kisasa na baada ya mavuno kampuni hiyo kununua mazao hayo.


Alisema mara baada ya kuwapatia mafunzo namna bora ya kuendesha kilimo kwa wakulima pindi wanapovuna mazao yao kampuni hiyo itanunua mazao hayo na kuyapeleka katika kiwanda chao kilichopo KIBAIGWA mkoani Dodoma kutengeneza bidhaa ambazo huuzwa kwa mawakala na wanachama wa Jatu waliopo nchi nzima kupitia mfumo wa biashara wa masoko ya mtandao(Network Marketing).


Alisema unaweza kuwa- mwanachama wa mteja kwa kujiunga Tsh 10,000 tu na kupewa namba ya utambulisho ya uanachama ili kuweza kununua bidhaa zetu na kupata gawio kila mwisho wa mwezi kutokana na manunuzi yako wewe na vizazi vyako


Pia Bw. GASAYA aliongeza kuwa kampuni hiyo inaongoza kwa kutoa huduma bora hili kuwezesha upatikanaji wa kipato kwa kila mtu imeanza kuuza hisa zake ambazo zinauzwa kwa Tsh 2,500 ambapo utapata gawio la faida la kila mwaka kutokana na Hisa zako.


Aidha Amezitaja faida za kujinga na kampuni ya JATU PLC pamoja na wanachama kusaidiwa kurasimishiwa ashara yake, kuunganishwa na mfuko wa bima ya afya, kupatiwa mafunzo ya ujasilimali, kupokea malipo kila mwezi kutokana na manunuzi yako pamoja na kuwa mwanachama wa SACCOS ya Jatu

No comments