MAHAKAMA KUU YAITOSA BODI YA LIPUMBA
Bodi ya Wadhamini iliyo chini ya
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,
Profesa Ibrahim Lipumba, imeiomba Mahakama Kuu iitendee haki kwa kuithibitisha
kama bodi halali ya chama hicho, ili iweze kufuta kesi zilizofunguliwa dhidi ya
Lipumba na wenzake, kwa madai zilifunguliwa na Bodi isiyo halali.
Wakati akizungumza na waandishi wa
habari, jana Julai 6, 2017 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Slaam , Katibu
wa Bodi hiyo, Thomas Malima alidai kuwa mahakama hiyo haikuwatendea haki kwa
kutothibitisha uhalali wa bodi hiyo pamoja na kutowatambua mawakili wake.
“Mahakama
haikutupa haki ya kutusilikiliza na kuithibitisha bodi yetu ambayo ni halali,
mawakili wanaojiita wa bodi ya CUF ndiyo wale tuliowafukuza kazi, ambao kwa
sasa ni sawa na mawakili wa mahakama na si wa chama chetu hatuwatambui, sisi
ndio wenye mamlaka ya kufuta kesi,” alisema Malima.
Aidha, Bodi ya Wadhamini iliyo chini
ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad imefungua mashauri takribani
sita dhidi ya Lipumba na wenzake ikiwemo shauri la kuzuia utolewaji wa fedha za
rudhuku ya chama hicho kwa Lipumba.
Na kwamba Bodi ya Lipumba inadai kuwa
kesi hizo zimefunguliwa kinyume na sheria kwa kuwa yenyewe ndiyo yenye uhalali
wa kufungua kesi za chama hicho.
No comments