URUSI YAITIMUA NDEGE YA NATO ILIYOKUWA IKIMFATIOLIA WAZIRI WAKE WA ULINZI.
Ndege ya kijeshi ya Urusi, Su-27 imefanikiwa
kuitimua ndege ya jeshi la NATO, F16 ambayo ilikuwa ikiifukuzia ndege aliyokuwa amepanda
waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu
Vyombo vya habari Urusi
vimesema kuwa tukio hilo limetokea katika anga ya kimataifa eneo la
Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda himaya ya Urusi ya
Kaliningrad.
NATO baadaye ilisema
ilifuatilia ndege hiyo kwa kuwa haikujitambulisha.
Kwa mujibu wa mashirika ya
habari ya Urusi ndege ya F16 ilipita karibu na ndege ya Waziri wa Ulinzi,
Shoigu, kisha ndege ya Urusi ya Su-27, ikaingilia kati na kutoa ishara
kuonyesha kuwa ilikuwa imejihami, kisha ndege ya Nato ikaondoka.
No comments