UJUMBE ALIOPOST MHE KIGWANGALLA: TULIOPINGA WIZI WA MADINI YETU TULIBEZWA, TULIKAMATWA KAMA WEZI
Kupitia
ukurasa wa kijamii wa twitter wa Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, ameweka wazi kuwa daima ataendelea kupambana dhidi ya rasilimali za
umma, kwani amekuwa mwanaharakati kwa muda mrefu.
“Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa
kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi?
#NasimamaNaRaisWangu” aliandika Dk. Kigwangalla huku watu mbalimbali
wakitoa maoni yao.
Kwa
mujibu wa Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, suala la kupambana na rasilimali za
Taifa alilianza miaka mingi kwani miongoni mwa matukio makubwa ni la 2013,
ambapo alijitolea kupambana kudai haki tukio lililopelekea kutiwa nguvuni
na Jeshi la Polisi.
Dk.
Kigwangalla anasema katika kupigania maslai Taifa ataendelea kuunga mkono
juhudi za Rais Dk. Magufuli mwanzo mwisho kwani ni moja ya matunda ya
nchi yoyote ile Duniani.
Anasema
kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali za nchi, hivyo akiwa
Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo bila kuchoka.
|
No comments