OLE SENDEKA AMPA TANO LOWASSA
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua
kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Acacia.
Ole
Sendeka ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesema kuwa baada
ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chadema amempongeza Rais, hana budi kumshukuru na kumpongeza pia
kwa kufanya hivyo, na kuwaomba wabunge wote bila kujali vyama vyao kumuunga
mkono Rais Magufuli kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi.
“Nanyi
wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea rasilimali
za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha Watanzania, waweze kupata
huduma zao za msingi kupitia madini hayo,” Ole Sendeka anakaririwa na
Mwananchi.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Njombe alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza jana kwenye
mazishi ya mama yake mzazi yaliyofanyika katika kijiji cha Losokonoi wilayani
Simanjiro.
Alimuomba
mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya ambaye alihudhuria mazishi hayo,
kumfikishia salamu na pongezi hizo kwa Lowassa.
Lowassa
alimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake baada ya kupokea ripoti ya pili ya
uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini yanayoshikiliwa na Serikali katika
bandari ya Dar es Salaam, yalipokuwa katika mchakato wa kusafirishwa nje ya
nchi na kampuni ya Acacia.
No comments