MAREKANI YAITUNGUA NDEGE YA KIJESHI YA SYRIA
Marekani imeitungua ndege ya kijeshi
ya Syria iliyokuwa ikijiandaa kuwashambulia wanamgambo wa IS ambao wamekuwa
wakihatarisha maisha ya wananchi wa nchi hiyo huku umoja wa mataifa ukitaka
kuwepo na usuluhishi.
Aidha, Marekani imesema kuwa imefikia
hatua hiyo mara baada ya jeshi la Syria kuvishambulia vikosi vya Syrian
Democratic Force SDF, vinavyoungwa mkono na Marekani kwa lengo la
kupambana na wanamgambo wa Islamic State.
Kwa upande wa Serikali ya Syria
imesema kuwa ndege yake ilikuwa katika maandalizi ya kuwashambulia wanamgambo
wa Islamic State na si vikosi vya Syrian Democratic Force vinavyoungwa mkono na
Marekani.
Vikosi vya Syrian Democratic Force
(SDF ) vinaungwa mkono na umoja unaoongozwa na Marekani kwaajili ya kupambana
na wanamgambo wa Islamic State ambao wamekuwa tishio katika ukanda huo.
No comments