MHE ALLY KESSY: WABUNGE WASUMBUA BUNGENI WAPIMWE MADAWA YA KULEVYA
Mbunge
wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya kuwapima
wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza
bungeni mara kwa mara.
Keissy
alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari
wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha
kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.
"Tutengeneze
sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya
kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge
letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge
haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale
yale" alisema Keissy na kuongeza;
"Adhabu
ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi
sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana
kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara
hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri
pamoja na cheo"
No comments