KAULI YA WAZIRI MKUU KWA MAFATAKI WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayebainika amemkatisha mwanafunzi
wa kike masomo kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya ukatili
vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka 30 jela.
Majaliwa
ametoa agizo hilo leo Lugalo jeshini Jijini Dar es Salaam wakati akizindua na
kukabidhi vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu
vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa ajili ya shule 1696 kwa
nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uboreshaji wa masomo ya sayansi.
Vilevile
Majaliwa ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha wanakamilisha maabara za shule zote
nchini 4587 ambazo bado hazijakamilika ili vifaa hivyo vianze kusaidia
wanafunzi kwa haraka na kufikia malengo ya nchi ya kuwa ya uchumi wa kati.
Pamoja
na hayo, Majaliwa amesema watendaji watakaoenda kinyume na maadili ya kazi zao
ni lazima mkono wa sheria uchukue nafasi yake.
No comments