KUALI ZA MHE LOWASSA, SUMAYE, MBATIA KATIKA MAZISHI YA NDESAMBURO
Na Regina Mkonde
Viongozi
wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa
Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga
mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki
ya kisiasa.
Katika hatua nyingine, wameshangazwa na CCM
kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki
dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya
KCMC Moshi.
Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti
demokrasia. “Nawapongeza kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada
za kudhibiti demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure."
Naye
mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “Hata njia za
kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai,
wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu ya amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea
kuzaa aliyoyasimamia.”
Wakati akitoa salamu hizo, Mwenyekiti mwenza
wa UKAWA, James Mbatia alisema kitendo cha viongozi wa CCM kutohudhuria kwenye
ibada hiyo si cha kiungwana kwani kinalenga kugawa wananchi kwa misingi ya
vyama.
“Walichofanya leo sio cha kiungwana,
watanzania tusikubali kugawanyishwa kwa misingi ya imani wala vyama, sijauona
uwakilishi wa CCM, tuwasamehe na mimi nimewakilisha CCM wote hapa ili tulete
amani ya mzee Ndesa.Ndesamburo alikuwa analeta watu wote pamoja, lakini leo
hata njia za kupitisha mwili wake nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe
hatutakua hai,” alisema.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti CUF Severina
Mwijage wakati akitoa salamu za rambirambi alisema amesikitishwa na kitendo cha
kuzuiwa uwanja kwani marehemu Ndesamburo alishiriki kuujenga uwanja huo.
“Siasa za sasa hivi ni hatari, za kupandikiza
watu chuki ni mbaya sana, na mimi naomba niongezeee wenyewe wanajua chuki ndio
chama chao kitakachosaidia kuchukua dola, sisi tunachaguliwa na wananchi
tunajua matatizo ya wananchi, aelewe yule anayewachonganisha itakuaje yeye
ambaye aliyemchagua atakuja na kuondoka na yeye atabaki katika mkoa na watoto
wake wanaishi na wananchi,” alisema.
No comments