HII NDIO KAULI YA MHE MBOWE KUFATIA SAUTI YAKE INAYOSAMBAA MITANDAONI IKIDAI WEMA SEPETU NI MPENZI WAKE
Habari inayotikisa
mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile Audio
(voice note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa
Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.
Leo kupitia 255 ya
XXL ya Clouds FM Mbowe ameielezea sauti
hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka:
“Mimi nalichukulia
kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa ambazo
zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema kwa sababu
siyo za kweli.
“Timu yangu ya
mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kutuchafua kwani
tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu.
"Sauti siyo ya
kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wetu na
kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za upotoshaji tu."
No comments