TGNP YATOA MAFUNZO KWA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU MIKATABA YA MALENGO ENDELEVU YA KITAIFA NA KIMATAIFA YA KIJINSIA .
Mtandao
wa jinsia Tanzania (TGNP) Imeandaa warsha ya mafunzo kwa asasi mbalimbali za kiraia
na wadau wa serikalni ili kujadili mchakato wa mikataba ya malengo endelevu ya kitaifa na kimataifa ya
kijinsia .
Akizungumza
jijini Dar es saalam Mkurugenzi mtendaji wa TGNP mtandao Bi.Lilian Liundi
amesema kuwa lengo ni kuangalia mikataba hiyo kama imekidhi mfumo wa kuondoa
ukandamizi dhidi ya wanawake katika kuleta maendeleo katika sekta ya maji,afya
na elimu na nafasi za uwiano katika uongozi baina ya mwanamke na mwanaume.
Bi.
Liundi amebainisha kuwa katika kuhakikisha maendeleo endelevu yanakuwepo ni
vema kwa wanaume kukubali kuwa sehemu ya mabadiliko kwa kinamama ili kuweza
kufikia malengo ya kimaendeleo ifikapo mwaka 2030.
Aidha
amesema kuwa katika masuala muhimu yanayojadiliwa ni pamoja na kuangalia bajeti
zinazosomwa endapo zimezingatia vigezo vya kuondokana na uonevu kwa wanawake
kama ndoa za utotoni,ukatili wa kijinsia na usawa wa madaraka baina ya mwanamke
na mwanaume.
Amesema
kuwa ni vema serikali na vyama vya siasa
nchini kutoa kipaumbele kwa wasiojiweza
na walemavu
Nae mshauri na mtaalam wa masuala ya jinsia wa
TGNP mtandao Bw. Edward Mhina amesema kuwa taswira inayotakiwa kufikia mwaka
2030 hedhi kwa watoto wa kike isiwe
kizuizi au sababu ya kukosa masomo.
Ameongeza
kuwa ni vema watoto wa kike na kiume kupata elimu ya msingi hadi chuo kikuu kwa
usawa pasipo ubaguzi wowote.
Amesema kuwa wanawake wamekuwa wakibeba mizigo kwa
makadirio ya tani tano kwa mwaka jambo ambalo kwa kuliangalia ni uonevu na
kandamizi kimfumo baina ya kike na kiume.
Mbali
na hayo amesema kuwa kuna haja ya kuangalia viashiria ili kuweza kushiriki kikamilifu katika
utekelezaji wa Tanzania ya viwanda ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo baina
ya jinsia.
Mafunzo
hayo ya siku tatu yameandaliwa na TGNP na kushirikisha wadau mbalimbali na
asasi zisizo za kiserikali yamelenga kuangalia mchakato wa mikataba ya
kimataifa ya kijinsia katika kuleta maendeleo.
No comments