HEINEKEN YAWAKUTANISHA WADAU JIJINI DAR KUSHUHUDIA FAINALI YA LIGI YA UEFA LIVE 2017
Michuano ya UEFA
Champion ligi 2017 imemalizika kwa timu ya Real Madrid kuibuka mshindi kwa
mabao 4 kwa 1 dhidi ya washindani wao wa timu yaJuventus.
Katika kuhakikisha
mashabiki wa UEFA ligi wanashuhudia fainali hiyo Heinkein Tanzania wamejumuika
na mashabiki wake pamoja na vyombo vya
habari katika kushuhudia mtanange huo huku wakiburudika na kinywaji bora duniani
cha Heinkein.
Akizungumza afisa uhusiano wa kampuni ya bia ya
Heinkein Bw. Bethuel Kinyori amesema kwa kutambua mchango wao pamoja na
kutokana na wao kuwa ndio wafadhili wakuu wa michuano ya uefa 2017 wameona ipo
haja ya kuwakutanisha wadau na mashabiki ili kuweza kushuhudia fainali hiyo
Katika fainali hiyo
mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo
timu ya Real Madrid iliibuka na ushindi wa wa magoli 4 kwa moja dhidi ya
juventus.
Kufuatia ushindi huo
timu ya real Madrid inaendelea kushikilia rekodi ya kuwa timu ambayo imechukua
kombe hilo mara nyingi zaidi katika historia ya michuano hiyo tangu kuanza.
Kwa upande wa
mashabiki na wadau wa Heineken Tanzania wametoa pongezi kwa viongozi wa kampuni
hiyo kwa kutambua na kuwakutanisha kuweza kushuhudia fainali hizo.
No comments