Breaking News

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) YAFUTULISHA WATEJA NA WADAU WAKE JIJINI DAR

Waziri Wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira mhe January Makamba akiongea kwa niaba ya makam wa Rais mhe Samia Suluhu Hasani katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) serena jijini dar es salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya mambo ya ndani Mhe Hameid Masauni Akizungumza katika Hafla ya futari Iliyoandaliwa na Benki ya watu wa Zanzibar kwa wateja na wadau wake katika hoteli ya serena jijini dar es salaam. 





Wadau na wateja wa benki ya watu wa Zanzibar waliojumuika katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya serena jijini dar es salaam
Bw Juma Mmanga Mshereheshaji katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya watu wa Zanzibar katika hotel ya serena jijini dar es salaam 



Dar es Salaam
Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) imejipanga kuboresha huduma zake nchini ambapo inatarajia kufungua tawi jipya makao makuu ya nchi mkoani dodoma ili kuongeza ufanisi zaidi wa kutoa huduma zake. 

Akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja na wadau wake katika hoteli ya Serena jijini dar es salaam mkurugenzi wa benki hiyo bwana Juma Amein Hafidhi alisema kwa kutambua mchango wa wateja wao wameandaa futari hiyo ili kuweza kuwakutanisha pamoja na kubadilishana mawazo. 

Alisema Katika kuhakikisha benki hiyo inaendelea kuwa bora katika utoaji na upatikanaji wa huduma zake Wameamua kuwakutanisha wateja  na wadau wao kwa lengo la kuonyesha upendo kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Bw hafidhi aliongeza kuwa tukio hili ni ibada kamili na jambo  la muhimu kipindi hiki kwa waislamu na kwa jamii yote kwani ni kipindi ambacho kila mmoja analo jukumu la kumwabudu na kumwomba mwenyezi mungu. 

Aidha Akizungumzia malengo na mikakati ya benki ya PBZ kwa mwaka huu alisema benki hiyo imejipanga kuanza kuboresha zaidi huduma zake kwa wateja ikiwa pamoja na kutoa mikopo ya ujenzi kwa wateja wake kisha kurejesha mikopo hiyo taratibu. 

Mapema akiongea kwa niaba ya wateja wa benki hiyo bw Massoud Khalifan ametoa pongezi kwa benki ya PBZ kwa kuwakumbuka na kuwaandalia futari kwan kitendo hicho kinaonyesha namna benki hiyo inatambua na kudhamini uwepo wao 

No comments