PICHA 16: MWENYEKITI WA WAENDESHA BODABODA MKOA WA SHINYANGA ALIVYOJINYONGA, CHANZO KIKIDAIWA NI MGOGORO KATI YA POLISI NA WAENDESHA BODABODA
Askari polisi wakiweka kwenye gari la polisi mwili wa
Mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki manispaa ya Shinyanga Jacob Paul
aliyejiua leo Juni 10,2017 kwa kujinyonga nyumbani kwake
|
Jacob Paul enzi za uhai wake
Kamanda wa jeshi la polisi ACP Muliro Jumanne Muliro
(wa tatu kutoka kushoto) akiwa nyumbani kwa marehemu Jacob Paul
Wananchi wakiwa nyumbani kwa marehemu
Jacob Paul
Kamanda wa jeshi la polisi ACP Muliro Jumanne Muliro
akisikiliza maelezo kutoka kwa mke wa marehemu,bi Rebeca Amos
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro
Jumanne Muliro akielekea kwenye chumba cha marehemu Jacob Paul akiwa
ameambatana na maafisa wa jeshi la polisi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa
Askari polisi wakiimarisha ulinzi
nyumbani kwa marehemu Jacob Paul
Mke wa marehemu akilia kwa uchungu wa
kupoteza mme
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Wananchi wakiwa nyumbani kwa marehemu
Jacob Paul
Askari polisi wakiwa wamebeba mwili wa
marehemu Jacob Paul
Askari polisi wakiondoka na mwili wa
marehemu
Jirani yake na marehemu,Sarah Edward
akielezea tukio hilo
Diwani
wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
tukio la mwenyekiti wa waendesha bodaboda manispaa ya Shinyanga,Jacob Paul
aliyejiua kwa kujinyonga
Shinyanga:
Askari Polisi Wakiweka Kwenye Gari La Polisi Mwili Wa
Mwenyekiti Wa Chama Cha Waendesha Pikipiki Manispaa Ya Shinyanga Jacob Paul
Aliyejiua Leo Juni 10,2017 Kwa Kujinyonga Nyumbani Kwake Huku Chanzo
Kikihusishwa Na Mgogoro Wa Waendesha Bodaboda Na Jeshi La Polisi Mkoa Wa Shinyanga
Mamia Ya Wakazi Wa Shinyanga Wamepigwa Butwaa Baada Ya
Mwenyekiti Wa Chama Cha Waendesha Pikipiki Maarufu Bodaboda Katika Manispaa Ya
Shinyanga Jacob Paul (36) Kujiua Kwa Kujinyonga Kwa Kutumia Waya Wa Simu Chumbani
Kwake.
Tukio Hilo La Kushangaza Limetokea Jumamosi Juni 10,2017
Majira Ya Saa Nane Mchana Katika Mtaa Wa Mwinamila Kata Ya Ngokolo Katika
Manispaa Ya Shinyanga.
Mashuhuda Wa Tukio Hilo Walisema Jacob Paul Ambaye Ni
Mwenyeji Wa Mkoa Wa Kigoma Alifika Nyumbani Kwake Leo Majira Ya Saa Saba Mchana
Akiwa Amepakizwa Kwenye Pikipiki Na Mwendesha Bodaboda Mwenzake Huku Akionekana
Kuwa Mtu Mwenye Furaha Kisha Akaingia Ndani Kwake.
Walieleza Kuwa Baada Ya Takribani Dakika 30 Watoto Wawili
Marehemu Walifika Nyumbani Wakitaka Kuingia Ndani Ya Nyumba Lakini Mlango
Ulikuwa Umefungwa Kwa Ndani Walijaribu Kumuita Lakini Hakujibu Ndipo Wakaamua
Kwenda Kuchungulia Dirishani.
Walifafanua Kuwa Watoto Hao Walipochungulia Dirishani
Walimuona Baba Yao Akiwa Amening’inia Chumbani Kisha Kutoa Taarifa Kwa Majirani
Na Baba Mwenye Nyumba Akaamua Kutoa Taarifa Kwa Jeshi La Polisi.
“Mke Wa Marehemu Hakuwepo Tulipoona Kuwa Mlango Ni Mgumu Kufunguka
Tuliamua Kuuvunja Na Kumkuta Amejiua Na Huenda Chanzo Cha Kifo Chake Kimetokana
Na Msongo Wa Mawazo Kwa Sababu Tangu Kutokea Kwa Tukio La Mwendesha Bodaboda
Joel Gabriel Mamla (26) Kufariki Dunia,Alikuwa Anasema Waendesha Bodaboda
Wenzake Wamekuwa Wakimlalamikia Kuwa Anashirikiana Na Polisi Kukamata Waendesha
Bodaboda Waliofanya Vurugu Hivi Karibuni”,Alieleza Jirani Sarah Edward.
“Jana Alikuwa Anasema Kuwa Anapewa Vitisho Na Wenzie Kuwa Anawasaliti Na
Kusababisha Waendesha Wakamatwe Na Polisi Na Pikipiki Zao”,Alieleza Jirani
Huyo.
“Nilikwambia Mme Wangu Ujiuzulu Uenyekiti,Ona Sasa Waendesha Bodaboda
Wenzako Wamekuponza,Wamekusababishe Ujiue Baba Joshua,Umeacha Familia Yako
Bora,Watoto Hawa Watalelewa Na Nani”, Mke Wa Marehemu Rebeca Amos Aliyekuwa Analia Muda Wote
Wakati Wa Tukio Alisikika Akiongea Kwa Uchungu.
Alisema Mme Wake Amekuwa Akipokea Vitisho Kwa Watu
Wasiojulikana Wakimtuhumu Kuwasaliti Na Kusababisha Wakamatwe.
Habari Kutoka Eneo La Tukio Zinasema Kuwa Marehemu Alikuwa
Analalamikiwa Na Waendesha Bodaboda Wenzake Kuwa Anashirikiana Na Jeshi La
Polisi Kugandamiza Waendesha Bodaboda Wenzake.
“Mwenyekiti Anadaiwa Kuwasaliti Wenzake,Hata Kipindi Kile Mwendesha
Bodaboda Boaz William Aliyefariki Dunia Kwa Kugongwa Gari Wakati Akidaiwa
Kuwakimbia Askari Wa Usalama Barabarani Mjini Shinyanga Anadaiwa Kushirikiana
Na Polisi Kutorosha Mwili Wa Marehemu Na Kuupeleka Kigoma Kwa Ajili Ya Mazishi
Ambapo Hata Waendesha Bodaboda Hawakupata Hata Nafasi Ya Kuaga Mwili Wa
Marehemu.
Diwani Wa Kata Ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi Alifika Eneo La
Tukio Alimuomba Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli Kuunda Tume Huru Ya Kijaji Kuchunguza Vifo Vya Waendesha Bodaboda
Katika Manispaa Ya Shinyanga.
“Sasa Idadi Ya Vifo Vya Waendesha Bodaboda Vimetokea Shinyanga,Kuna Utata
Kwani Jamii Inasema Vifo Vinasababishwa Na Askari Polisi Huku Jeshi La Polisi
Nalo Likidai Waendesha Bodaboda Ndiyo Wanasababisha Vifo Vyao Kwa Kukiuka
Sheria Za Usalama Barabarani,Mpaka Sasa Pikipiki Nyingi Zimekamatwa”,Alieleza Ntobi.
Kamanda Wa Jeshi La Polisi Acp Muliro Jumanne Muliro
Aliyekuwepo Eneo La Tukio Alisema Wamekuta Mwenyekiti Huyo Wa Waendesha
Bodaboda Amejinyonga Kwa Kutumia Waya Mgumu Wa Simu Katika Chumba Chake.
“Tumepata Taarifa Kuhusu Tukio Hili,Tulipofika Tumekuta Amefariki Kwa
Kujing’iniza Kwa Waya,Tumeuchua Mwili Wa Marehemu Kwa Ajili Ya Kuufanyia
Uchunguzi Hospitalini,Sisi Kazi Yetu Ni Kuchunguza Chanzo Cha Kifo,Bado
Tunafanya Uchunguzi Zaidi Juu Ya Tukio Hili Tutatoa Taarifa Zaidi Baadaye”,Alisema Kamanda
Muliro.
Tukio La Mwenyekiti Wa Waendesha Bodaboda Kujiua Limetokea
Siku Tano Tu Baada Ya Jeshi La Polisi Mkoani Shinyanga,Kulazimika Kuwapiga
Mabomu Ya Machozi Waendesha Bodaboda, Kwa Kitendo Cha Kuundamana Kupinga Kifo
Cha Mwenzao Joel Gabriel Mamla (26),Kilichodaiwa Kusababishwa Na Askari Polisi
Pc Edmund Baada Ya Kumkamata Kwa Kosa La Kutovaa Helmet.
Kwa Mujibu Wa Jeshi La Polisi Watu 26 Walifikishwa Katika
Mahakama Ya Wilaya Ya Shinyanga Kwa Mashtaka Ya Kufanya Mkusanyiko Usio
Halali,Kufanya Fujo Na Kujaribu Kufanya Maandamano Kinyume Na Sheria.
Kati Yao David Laurent Alikiri Kosa Lake Na Kuhukumiwa
Kifungo Cha Miezi Sita Jela Na Wengine Kesi Yao Iliahirishwa Na Itaendelea
Julai 23,2017.
Hii Hapa Taarifa Ya Jeshi La Polisi Kuhusu Waendesha
Bodaboda Kufikishwa Mahakamani.
Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Shinyanga Kwa Vyombo Vya
Habari Tarehe 10/06/2017
Tarehe 09/06/2017 Watu 26 Walifikishhwa Katika Mahakama Ya
Wilaya Ya Shinyanga Na Kufunguliwa Kesi Ya Jinai No 134 Na Baadae Kusomewa
Mashitaka Ya Kufanya Mkusanyiko Usiohalali , Kufanya Fujo Na Kujaribu Kufanya
Maandamano Kinyume Na Sheria.
Makosa Hayo Waliyatenda Tarehe 07/06/2017 Majira Ya Saa
04.30 Asubuhi Wakati Kundi La Watu Wapatao 80 Wengi Wao Wakiwa Ni Waendesha
Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Wakiwa Eneo La Ibinzamata Manispaa Ya Shinyanga
Kwa Pamoja Walikusanyika Wakapanga Na Kufanya Maandamano Kinyume Na Sheria Na
Kuanza Kuyarushia Mawe Baadhi Ya Magari Na Kusababisha Usumbufu Kwa Baadhi Ya
Raia Na Watumiaji Wengine Wa Barabara Na Hivyo Kujenga Hofu Na Kupelekea
Kuvunjika Kwa Amani Katika Eneo Hilo.
Mtuhumiwa Mmoja No 18 Katika Hati Hiyo Ya Mashitaka Aitwaye
David Laurent Alikiri Kosa Lake Baada Ya Kusomewa Mashtaka Hayo Na Mwanasheria
Wa Serikali Caroline Mushi Mbele Ya Hakimu Denis Luwungo.
Mtuhumiwa Huyo Amehukumiwa Kifungo Cha Miezi Sita Jela Na
Wengine Kesi Yao Imeahirishwa Na Itaendelea Tarehe 23/06/2017.
Wakati Huohuo Imetokea Ajali Ya Pikipiki Na Kusababisha
Kifo. Tarehe 10/06/2017 Saa 08 Usiku Barabara Ya Maganzo Eneo La Matanda Sisi
Kwa Sisi Zone 1 Mwendesha Pikipiki Shinje Machiya Mkazi Wa Bugweto Akiwa Na
Pikipiki No Mc 303 Huku Akiiendesha Kwa Kasi Na Bila Kuwa Na Kofia Ngumu Helmet
Alipata Ajali Baada Ya Kuanguka Na Kufariki Palepale Baada Ya Kuvuja Damu
Nyingi Kichwani.
Chanzo Cha Kifo Hicho Ni Mwendo Kasi , Kutovaa Helmet Na
Kupelekea Ajali Iliyosababisha Kuvuja Kwa Damu Nyingi Kichwani Na Hatimaye
Kufa. Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Shinyanga.
Imetolewa Na Muliro J Muliro (Acp) - Rpc Shinyanga.
Source Malunde1
blog
No comments