WAZIRI MWIJAGE: WATANZANIA TUJIVUNIE KUNUNUA BIDHAA ZINAZOZALISHA NCHINI.
Waziri Mwijage Akizungumza katika halfa ya ufunguzi wa duka kubwa la vifaa vya ujenzi
Balozi wa china Tanzania dkt LU Youqing akizungumza katika unguzi wa duka
hilo
Bidhaa zinzazopatikana katika duka hilo
Wazri Mwigaje akisikiliza maelekezo kutoka kwa
moja wa viongozi wa duka hilo
Waziri Mwijage akitoka katika duka hilo mara baada
ya ukaguzi
Wazri Mwigaje akikata utepe kuashiria kufunguliwa
kwa duka hilo.
Waziri wa viwanda na
biashara Mhe Charles Mwijage amefungua rasmi jengo la kampuni ya Taifa ya vifaa
vya ujenzi la China National Building Material Group Limited (CNBM) lililopo
mikocheni jijini Dar es salaam.
Akizungumza halfa ya
ufunguzi huo mhe Mwijage alisema kampuni hiyo ni ya kimataifa na yenye viwango
imejenga zaidi ya asilimia 65 ya viwanda vyote vya saruji na vioo duniani.
Waziri Mwijage alisema
kampuni ya CNBM ina uwezo mkubwa katika uzalishaji wa cement na imekuwa
ikizalisha tani 530 milioni kwa mwaka wakati uwezo wa Tanzania katika viwanda
vilivyosimikwa ni tani milioni 10.8 na kubainisha kuwa kiasi kinachohitajika
nchini ni tani milioni 4.8.
Ameongeza kuwa CNBM
inatarajiwa kushirikiana na mwekezaji mwingine ambaye anakwenda kujenga kiwanda
Tanga kitakachozalisha tani milioni saba
za cement na kubainisha kuwa hakuna kiwanda kinachozalisha tani milioni saba
Tanzania.
Aidha mhe Mwijage aliongeza
kuwa CNBM kwa kutambua umuhimu wa
uwekezaji na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi hapa wamekuwa wakitoa maelekezo kwa
wataalam nchini badala ya kununua vifaa
hivyo nje ya nchi.
Kwa upande wake
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. alisema urafiki baina ya China na Tanzania ni wa kihistoria tangu kwa
Rais Xi Jinping ambapo urafiki huo umekuwa
mwendelezo hadi kwa serikali ya
awamu ya tano ya Rais John Magufuli.
Nae Mkurugenzi wa
China National Building Material Group Limited
(CNMB) Bw. Andy Chen amesema
kampuni hiyo inatoa fursa ya kazi kwa watanzania pamoja na kutoa mafunzo
yatakayowasaidia kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.