TCRA YATOA TAADHALI KWA WATUMIAJI WA KOMPYUTA JUU YA SHAMBULIO LA KIRUSI KIITWACHO WANNACRY
Shambulizi
la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka
kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.
Kampuni
ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za
programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry'
duniani.
Kuna
ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati
ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza
na Uskochi.
Programu
hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili
kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.Siku nzima, mataifa ya
Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.
==>
Hii ni Tahadhari Iliyotolewa na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuhusu
Kirusi hicho
No comments